Mwenyekiti wa Kamatiya Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF), Elias Mwanjala amesema kesi ya Bernard Morrison itaendelea kuskilizwa kesho.
Kiungo wa Yanga, Morrison alikuwa na mvutano mkubwa na klabu ya yake kuhusu sakata la mkataba ambapo yeye anadai kwamba ana dili la miezi sita ambalo limekwisha huku Yanga ikieleza kuwa ana dili la miaka miwili.

Sakata lake leo ni siku ya pili ambapo lilianza kusikilizwa jana, Agosti 10 na leo Agosti 11 pia limeskilizwa na hakuna majibu ambayo yametolewa.
Mwanjala amesema kuwa kuna document moja haijakamilika kwa pande zote mbili ya Yanga na Morrison na pande zote zimesema jioni ya leo watazileta.

“Kuna nyaraka ambazo hazijakamilika kwa pande zote mbili, moja ya Yanga na moja ya Morrison jambo ambalo limefanya tushindwe kutoa maamuzi.
“Kesho zitakabidhiwa kwa kamati ambapo kikao kitaanza kesho saa 4 asubuhi kufikia saa saba na nusu kesho kikao kitakuwa kimekwisha na watatoa maamuzi juu ya kesi hiyo.”
Morrison Agosti 8 kesi yake ikiwa bado haijatolewa hukumu alitambulishwa na watani wa jadi Simba huku ikielezwa kuwa amesaini kandarasi ya miaka miwili jambo linaloongeza mvutano wa uhalali wake.

Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Gabriel
Hapa Elias mwanjala anashindwa kusema kwel maana hili swala maamuz ni Jambo rahisi sana maana uwez ukamchukua mfanyakaz toka labda singida kwa dhamana ya wazaz wa huyo mfanyakaz alafu akafanye Kaz pengne kwa tamaa zake tu hapo swali akipata tatizo litakuwa la nan? Kwa upande wa Morrison huyo n Mali ya yanga ata akafanye vip bado anamkataba wa dhamana ya migration kutoka yanga kwahiyo tatizo lolote likitokea lazma atahusika yanga japo amesain Simba cha msingi arudishwe kwao tu au Simba wavunje mikataba yote ya dhamana ya makaz ambayo alisain ndan ya miaka miwili maana hapa TFF lazma waje kuulizwa kwann uliamua kukubal kumsainsha mchezaj bila kufuata utaratibu maana TFF n wazembe hawako Makin
Shafii
Wadau wa soka tunasubili maamuzi yatakayo tolewa na uongozi tujue ni mchezaji wa club gani.
Povel
Ngoj tusubir kesho hyo
Adelta
Wadau tunasubir majibu yanayotolewa
Amani
Tanzania mpira bado sana
Saupha mohamed
Tusibili tuone
Fatina mfingi
Mmh hii hatar ngoj tusubir
Dorophina
Morrison anazingua wampige chini arudi kwao kabisa
Khadija
Tanzania mpira bado sana#meridianbettz
Zeiyana
Morrison kazingua tu kuikweli siku zote mtu hauwezi kumzarau boss wako aliyekutoa kwenu akakuleta mjini hinaonekana hiyo ndio tabia yake kama ni vipi harudushwe kwao tu hapeleke mbele zarau zake
Mwajumah
Ngoja tusubili kesho iyo#Meridianbettz
Sadick
Kumekuwa na tatizo kwenye eneo hili hapa nchini la viongozi na wachezaji kutokuwa na mikataba ya wazi hivyo kupelekea kutohemiwa#meridianbettz
Caroline
Si watoe tu hukumu ya iyo kesi.mara leo Mara kesho.mbona hatuwaelewi
felister
wadau wa soka wasubiri waone mamuzi yatakayotolewa
David Pere
TFF wanatuchanya watoe maamuzi watu wakeww Kama nini kinaendelea
Njiku
Mpira wetu wa bongo na viongozi wa vilabu hii vikubwa viwili hawajielewi kabisa wanachotakiwa kufanya kushindani kimataifa na sio wao kwa wao hii inshu ya morrision hahaha sijui maana wanaleteana uwasama tu
aisha
Tupo makini na swala hili tunasubili majibu ili tufahamu atakuwa club gani
Sylvester
Bongo ujanja ujanja mwingi sanaaa kwa kifupi nachukia mfumo wote kwa ujumla unaotumika
Tatu
Huu mchezo awitaji hasira tuendelee kula mtori nyama tutazikuta chini ishu ya merrison sio ya kitoto
Ester jackson
Hatari aende kwao mana hakuna mtoto anaye mzidi mzazi wake aliye mleta duniani
Rehema
Goja tuona iyo kesho itakuwaje
Salma ngende
Tunasubiri mwisho wa hili
Neema
Mmmmh kazi kweli kwelii
Leonard
Tff wao ndio watutegulie hiki kitendawili
Nasra
Inapaswa tuwe wavumilivu tusubili maamuzi kutoka kwenye uwongozi.
Devotha
Kipindi cha usajili bongo kinanoga sana kuliko ligi! Ngoja tusubiri na tuone nini hatima yake
Sabrina
Morrison kayakanyaga
Shan
Twasubir mahumuzi!
Fatuma kasomo
Ngoja tuone
Theonestina
Muafaka lazma upatikane.tunangojea matokeo
Rose kapinga
Duuuh hatar
Ernest
Yanga itakuja kuumbuka mwisho wa siku, Morrison kama Proffesional player hawezi kuact kama hivi pasipo sababu ya msingi
Furahav
Daah majanga.
magdalena
morrison alikuwa na uhakika wa kitu ambacho alikifanya hakukurupuka
warda
Huyu Morrison kama analazimishwa kucheza yanga ila sio mpenzi