Italia hawajapoteza mchezo wowote tangu October 2018, tumeruhusu mabao 7 tu kwenye mechi 27 na kama watu wanasema tunajilinda sana basi jueni tumefunga mabao 75, imagine
Licha ya huu ubora mkubwa niwakumbushe watu kuwa ni kazi nzuri za Academy, Vijana wengi chipukizi Italy wamepitia Atalanta Bergamo “La Dea” au The Goddess of Italiana Football, tumepambana kufika hapa
Usisahau na Project ya Sicily Projecto di Italia, Mikono ya Magodfather wa soka kama Roberto Mancini, Gianluca Viali na mafundi wengine wa zamani walioungana kusuka project ya One Italy!
Sasa kwenye bench la Ufundi la Italy kuelekea Euro ndipo kisa cha kusikitisha kilipo, Kocha Mkuu ni Roberto Mancini, Msaidizi wake ni Atilio Lombardo, wengine ni Alberto Evani na Fausto Salsano, huyo Atilio walikiwa wote tangu Man City
Kwenye bench lao kuna Jina la Gianluca Viali nyota na Kocha za zamani wa Chelsea! Huyu ameenda kama Mjumbe na Mshauri wa Mancini kwenye Italia yetu, ila huyu ndio sehemu ya huzuni, na Italia itafanya kila kitu tushinde EURO kwa ajili yake
Viali aligundulika na cancer ya Kongosho miaka minne nyuma, afya yake haipo sawa sana licha ya kuwa 2020 aliambiwa ameshinda vita ila bado anadai kiafya sasa hivi ni kama inamrudia tena
“Nina vita kubwa sana dhidi ya Adui Cancer, Adui ambaye ana nguvu zaidi yangu, tayari amepanda kwenye treni langu, nachoweza kufanya ni kusafiri nae kwa utulivu, labda siku moja atashuka na kuniacha niishi maisha yangu” hii ni stori ya Viali alipohojiwa kuhusu Cancer
Mancini, Lombardo na Viali wote wanafahamiana tangu wakiwa Sampdoria walicheza wote, sasa wanaelekea kwenye mission ngumu ya kutuvusha Italia, huku Wachezaji wakisema watafanya kila kitu kwa ajili yake
Viali amewaambia Wachezaji kama watashinda hii EURO basi hata kama Cancer itamuondoa basi atakufa huku akitabasamu, anaomba Mungu amfikishe mpaka fainali akiwa sehemu ya historia hii adhimu.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.
Asante kwa taarifa