Mchezaji nyota wa Manchester City ambaye ni nguvu ya pekee sana ndani ya kikosi cha Pep bado amekuwa gumzo ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani ndani ya kipindi hiki baada ya kocha wa kikosi hicho kuamini sana matumizi ya vijana ili kuwazoesha kwa ajili ya mashindano makubwa yajayo.
Nyota huyo amekuwa nguzo kubwa sana ndani ya kikosi hicho kwa kipindi cha hivi karibu baada ya hapo awali kuugulia maumivu ya kutemwa katika kikosi hicho lakini jambo hilo linaonekana kumjenga zaidi nyota huyo kutokana na kuonekana kama nguzo ya Ujerumani.
Hivi karibuni klabu ya Bayern Munich imekuwa ikihusika kwa namna moja au nyingine kutaka kumuweka nyota huyo nyumbani kwao kwa wakati ambao wamevutiwa sana na kiwango chake. Uwezo wake ndiyo unaomuweka sokoni kwa kipindi hiki baada ya kukaa kwa wakati mrefu bila kusajili.
Kwa hakika nyota huyo akijiunga na klabu hiyo ataweza kuifikisha kwenye mafanikio makubwa sana. Hata hivyo bado kuna ugumu kama Pep ataridhia kumuachia nyota huyo aondoke kikosini hapo baada ya kuona kwamba ana matumizi na nyota huyo kwa hapo baadaye maana hata umri bado unampa nafasi zaidi.
Hata ndani ya kikosi hicho kwa msimu huu hajawa na nafasi kubwa sana tofauti na msimu uliopita, ameanzishwa mechi chache sana ndani ya kikosi hicho cha matajiri wa Uingereza kwa hiyo hata akiondoka bado atakuwa na uhakika wa kucheza wakati wote.
Ameanza katika mechi 21 pekee ndani ya kikosi hicho ambazo ni mechi chache zaidi ya msimu uliopita ikiwa ni pungufu ya mechi sita ambazo msimu uliopita alicheza. Pia, ndani ya mechi hizo amecheza dakika chache sana ambazo kwa hakika hazilingani na zile za msimu uliopita.
Hata alipoulizwa juu ya usajili wake ndani ya klabu hiyo hajataka kabisa kulisemea ila kwa muonekano wake anaonekana kabisa kwa sasa hana maisha marefu kwenye klabu hiyo na anasema kila kitu kitafahamika baada ya mapumziko ya ligi kukamilika. Alijiunga na City kutoka Schalke mwaka 2016 kwa uhamisho uliogharimu kiasi cha £37m.


Mariam mtandama
Asante kwa taarifa meridianbet
Zeiyana
Pep hawezi kumacha sane haondoke
Povel tz
Habar njema