Raisi wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amekanusha taarifa zilizokuwa zinasambaa kwa kasi kuwa klabu hiyo inamradhimisha kiungo wa kimataifa wa Uholanzi De Jong kuondoka kwenye klabu hiyo.

De Jong amekuwa kwenye rada ya klabu ya Manchester United na wapo tayari kulipa kiasi cha €85milioni ili kuweza kuhakikisha wanapata huduma ya kiungo huyo, lakini wakala wa mchezaji huyo alitoa waraka kuwa De Jong hawezi kuondoka Barcelona na hayuko tayari kupunguza kiasi cha mshahara wake.

Joan Laporta

Joan Laporta alielezea kwa upande kuwa ikiwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anataka kubaki kwenye klabu hiyo, basi itabidi akubali kupunguza kiasi chake cha mshahara.

Taarifa iliyotolewa na mtandao wa Marca ulimnukuu Joan Laporta akisema, sio kweli tunaradhimisha kuuzwa kwa Frenkie de Jong, hiyo sio kweli.

“Frenkie safari ya Marekani itaamuliwa na Xavi na nafahamu atasafiri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa