Kiungo nyota wa klabu ya Manchester City Riyad Mahrez amesaini kandarasi ya kubakia kwenye viunga vya klabu hiyo hadi mwaka 2025.

Riyad Mahrez alisajiriwa na klabu ya Manchester City mwaka 2018 akitokea klabu ya Leicester City kwenye uhamisho uliogharimu kiasi cha £60 million, tangu asajiriwe amefanikiwa kucheza michezo 189, na kufanikiwa kufunga magoli 63, na kusaidia kupatikana magolli 43 kwenye mashindano yote.

Mahrez

“Nina furaha kubwa kuweza kusaini mkataba mpya. Nimekuwa nikifurahia kila dakika kwenye muda wangu hapa. Ni fahari kuwa sehemu ya klabu bora isioelezeka.” Alisema Riyad

Riyad kwenye miaka yake minne aliyotumia kwenye klabu ya City, amefanikiwa kushinda mataji manne ya ligi kuu ya uingereza, makombe matatu ya ligi na kombe la FA Cup moja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa