Raisi wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amesema kuwa Frenkie de Jong hauzwi na atafanya kila liwezekano ili kuhakikisha anambakisha kwenye viunga vya Camp Nou na kutangaza nia ya klabu hiyo kuwa hawako tayari kumuweka sokoni.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa zilizosibitisha kuwa, klabu ya Barcelona iko tayari kupokea kiasi kuanzia €65m hadi €80m kutoka klabu ya Manchester United ili kuweza kufanikisha uhamisho huo.

Joan Laporta

Lakini cha kushangaza, raisi wa klabu hiyo katoka hadharani na kusema hayuko tayari kumuachia mchezaji huyo wa kimataifa kutoka nchini Uholanzi, Joan Laporta kwenye kumbukumbu ya hayati Johan Cruyff alinukuliwa akisema.

“Nitafanya kila niwezalo ambalo liko ndani ya uwezo wangu kwa Frenkie kubaki, lakini pia swala la mshahara wake nitaliweka sawa.”


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa