Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesaini mkataba mpya na klabu ya Liverpool wa miaka miwili ambao utamuweka kwenye klabu hiyo hadi 2026.
Jurgen Klopp aliyejiunga na klabu hiyo mwaka 2015, awali alipanga kupumzika baada ya mkataba wake na klabu ya Liverpool kuisha, ambao ulikuwa unaisha mwaka 2024. Lakini mjerumani huyo hivi karibuni alionesha nia ya kutaka kuendelea kabaki kwenye dimba la Anfield na tayari ameshasaini mkataba mpya pamoja na wasaidizi wake Pep Lijnders na Peter Krawietz.

Hii ni habari njema kwa klabu ya Liverpool ambayo imepata uhai tokea apokee kijiti cha kuifundisha klabu hiyo ndani ya miaka saba aliyokuwepo kwenye klabu hiyo. Klopp kwa sasa ameshafanikiwa kuchukua ubingwa wa Carabao Cup, na anatarajia kucheza fainali ya FA Cup dhdi ya Chelsea.
Pia Klopp bado yuko kwenye mashindano ya Ulaya kwenye hatua ya nusu fainali na amecheza mschezo wake dhidi ya Villarreal siku ya jumatano na ameshinda 2-0, na bado kwenye ligi kuu ya Uingereza anashika nafasi ya pili huku akiwa nyuma kwa pointi moja dhidi ya kinara Man City.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.