Juventus: Chiellini Hatastaafu Msimu Huu!

Beki wa Juventus Giorgio Chiellini ameamua kuwa ataendelea kucheza soka, lakini Juventus bado hawajampatia mkataba mpya kusalia dimbani Allianz.

Kwa mujibu wa Corriere di Torino, nahodha huyu wa Juventus ameamua kuendelea na soka, hatastaafu kucheza mwisho wa msimu.

Kwa mujibu wa chapisho hilo, staa huyu anajiona yupo kwenye nafasi nzuri ya kuanza msimu mpya licha ya mkataba wake kuwa unaisha mwezi Juni.

Hata hivyo, awali taarifa zilitaja kuwa bila kupewa mkataba mpya na Juventus staa huyu hatarajii kucheza soka klavbu nyingine yeyote nje ya Italia au Ulaya.

Vieri: Chiellini ni Nguzo ya Juventus
Giorgio Chiellini

Baada ya kubadili msimamo, kuna fununu kuwa nyota huyu ataelekea Amerika Kaskazini au Marekani. Nyota huyu wa miaka 36 amecheza jumla ya mechi 14 msimu huu, na amecheza jumla ya mechi 531 kwa Juventus.

Chiellini amecheza mechi 106 na timu ya taifa ya Italia, aliwasili Julai 2005 akitokea Fiorentina. Amekuwa na mchango muhimu kwa klabu kushinda mataji tisa ya Serie A, nne ya Coppa Italia na matano ya Supercoppa Italiana.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

CHEZA HAPA

10 Komentara

    Giorgio Chiellini yuko vizuri ni bora abaki tu

    Jibu

    Wampe tu mkataba mpya

    Jibu

    Uongozi kama wanamuona bado anaweza kufanya vizuri wamuongezee mkataba#meridianbett#

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Bek makin sana

    Jibu

    Abaki tu yupo vyema sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Kazi kazi

    Jibu

    Juve wamuongezee tu mkataba mwingine kijana yupo vizuri

    Jibu

    Safiii sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.