Juventus wanataka kumsajili winga wa United Jadon Sancho ambaye hana mawasiliano mazuri na klabu yake mwezi Januari.
Ripoti kutoka gazeti la The Sun linaonyesha kuwa wababe hao wa Serie A wana nia ya kutaka kumnunua kwa mkopo wakati wa dirisha la katikati mwa msimu huu kwa nia ya kufanya dili hilo kuwa la kudumu kwa pauni milioni 60 msimu ujao.
Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.
Siku za Sancho Old Trafford zinaonekana kuhesabika, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa akifanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu baada ya kutofautiana hadharani na meneja Erik ten Hag.
United wanafikiriwa kutaka kumtoa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza na Juventus wanatumai timu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza itakubali kulipa nusu ya mshahara wake ikiwa atahamia kwa muda kwenda Turin.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Borussia Dortmund walidhaniwa kuwa ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kutaka kumsajili tena mshambuliaji huyo, baada ya kukaa miaka minne kwenye kikosi cha Bundesliga kabla ya kuhamia Theatre of Dreams mwaka 2021 kwa pauni milioni 73.
Lakini Sancho hana nia ya kurejea katika klabu yake ya zamani na anahisi kujenga upya wasifu wake nchini Italia kunavutia zaidi.
Muda wa Sancho huko United ulikuwa wa kusikitisha bila shaka, akiwa amefunga mabao 12 pekee katika mechi 82 alizocheza.