Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Mwina Kaduguda amesema sakata nyota wao wazamani Shiza kufungiwa miezi sita huku wao wakipigwa faini watalitolea ufafanuzi baada ya Bodi yao kukutana.
Jana kulitoka taarifa kutoka Shirikisho la soka Duniani (FIFA) kumfungia Kichuya miezi sita huku Simba ikipigwa faini ya dola 130,000 ni zaidi ya Shilingi Milioni 300 kwa kuondoka timu ya Pharco ya Misri bila kutoa taarifa kwa uongozi na hakupewa barua ya ruhusa (Release Letter).
Kaduguda amesema Bodi yao yenye watu 17 ikikutana anaamini suala hilo halitakuwa kubwa na amewataka wanachama na wapenzi wa Simba watulie wasubiri maamuzi ya Viongozi.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa kwenye sakata hilo huenda wao wakawa hawana kosa lolote hivyo watapeleka utetezi wao na kwa uzoefu wake kila kitu kitakaa sawa.
“Hili suala tumelisikia, tunasubiri Mtendaji wetu mkuu alilete kwenye Bodi lijadiliwe na ni matumaini yetu litamalizika vizuri kwakua tuna watu imara wa kufanya hilo,” amesema Kaduguda.
MALIZA MWAKA KIBINGWA KWA KUJISHINDIA SHEA YAKO KWENYE SHILINGI 140,000,000TSH!!
Kipindi hiki cha sikukuu kinamalizika kwa namna ya kipekee. Shilingi 140,000,000 kushindaniwa katika michezo ya Evolution kwenye Kasino Mubashara ya Meridanbet. Ingia mchezoni na ujiwekee nafasi ya kushinda shea yako!!!
Adelta
Hilo ni kosa ya kichuya mwenyewe
Shakila mrope
Iyo adhabu ni ya huyo kichuya
Issa
Kichuya ni moto
Sarah
Mwenye kosa nikichuya
Neema
Mambo ya adhabu sio poa kabisaa
Fatina mfingi
Duuh sio powah
Caroline
Walipe tu.no way out
Saupha mohamed
Dhuuu amna jinsi
Fatuma kasomo
Amna namna
Hopemwaikuka
Yupo huyoo
Tatu
Kichuya ndio ana makosa
Lydia Emmanuel Magoti
Duu siyo poa mjanga hayo
warda
Duu pesa nyingi mbona huyu Kichuya katuletea mambo meusi
Povel
Duh majanga kwl
aisha
Poleni sana wana simbaa maana hilo ni balaa kubwa sana
Dorophina
Kichuya ameiweka klabu matatani kwa kosa lake