Klopp Afiwa na Mama Yake Mzazi.


Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amepata pigo baada ya kufiwa na mama yake mzazi, Elisabeth aliyefariki jana Jumatano, februari 10, 2021.

Jurgen hataweza kuhudhuria mazishi ya mama yake nchini Ujerumani, kutokana na masharti makali yaliyowekwa na Ujerumani katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Covid 19.

 

“Alikuwa ndiyo kila kitu kwangu, alikuwa mama bora sana kwangu, kwa kuwa mimi ni Mkristo, naamini atakuwa sehemu bora peponi, ” amenukuliwa Kocha huyo na kuongeza kwamba maambukizi ya Corona yatakapotulia, amepanga kufanya hafla ya kipekee kumuenzi mama yake huyo.

Elisabeth na mumewe Norbert Klopp aliyefariki mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 66, walifanikiwa kupata watoto watatu, Stefanie, Isolde na Jurgen.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter, Klabu ya Liverpool imetoa salamu za rambirambi kwa kocha huyo kwa kumsindikiza na maneno ‘You will never walk alone Klopp’ na kusindikizia na alama ya kopa, ukiwa na maana kwamba Klopp hayupo peke yake katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mama yake.


TENGENEZA MKWANJA UKIWA NA MERIDIANBET 

Unaweza kuvuna mkwanja mrefu kadiri uwezavyo kupitia mchezo wa Gold n Rocks kwenye  kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Ni rahisi! Vigezo na masharti, kuzingatiwa.

SOMA ZAIDI

17 Komentara

    Pole Sana Klopp

    Jibu

    Klopp pole kwa kipindi kigumu

    Jibu

    Ni jambo gumu sana kufiwa na Mama yako na kushindwa kuhudhuria mazishi yake. RIP Mama Klopp.

    Jibu

    Dar pole sana klopp kwa msiba mzito

    Jibu

    Daah pole yake kloop

    Jibu

    Pole yake klopp pigo kubwa amepata

    Jibu

    Pole yake klopp
    Mama pumzika kwa amani 😭😭

    Jibu

    Pole sana R.I.P

    Jibu

    Pole sana Klop kwa msiba mkubwa uliokukuta

    Jibu

    Pole jurgen pigo sana

    Jibu

    So sad

    Jibu

    Pole sana Klopp

    Jibu

    Pole yake klopp

    Jibu

    Pole zimfikie klopp

    Jibu

    Pole sana klopp

    Jibu

    Polen sana

    Jibu

    Pole yake jamani

    Jibu

Acha ujumbe