Makocha wa vilabu vya Liverpool na Manchester United Jurgen Klopp na Erik Ten Hag wameamua kuungana ili kuhakikisha wanakomesha vitendo vya mashabiki wa vilabu hivo kuimba nyimbo za msiba katika mchezo unaozikutanisha timu hizo.

Klabu ya Liverpool itaikaribisha klabu ya Manchester United kesho katika dimba la Anfield lakini kocha Klopp na Ten Hag wameoongea na waandishi wa habari na kusema hawataki nyimbo za kutaniana kuhusu vifo baina ya vilabu hivo ziendelee kesho, Kwani michezo kadhaa iliyopita ya vilabu hivo ilitokea hali hiyo.kloppMiaka mingi iliyopita klabu ya Liverpool ilipata majanga na mashabiki wake kufariki ajali inayofahamika kama Hillsborough, Hivo mashabiki wa Manchester United wanatumia kama sehemu ya kuwatania klabu ya Liverpool na Liverpool wanawatania United kupitia ajali ya Munich ambapo klabu hiyo ikipoteza karibu wachezaji wake wote kwenye ajali ya ndege.

Kocha Ten Hag alisema kua anatambua kua mchezo kati ya Liverpool na Manchester United ni mchezo mkubwa na unaoteka hisia za mashabiki, Lakini haipaswi kutumia hasara ya maisha ili kupata alama na anaona ni wakati sahihi wa mashabiki wa timu hizo mbili kuachana na jambo hilo.kloppKocha Klopp Vilevile anatambua kua mchezo baina ya vilabu hivo ni mchezo mkali na mkubwa sana na hakuna ambae anaweza kufuta hilo, Lakini mambo ambayo yanapaswa kuachwa na mashabiki wa vilabu kuacha kuvuka mipaka ambayo inatoka nje ya uanamichezo na kusababisha hisia tofauti.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa