Beki wa klabu ya Manchester United Luke Shaw amesema kua ushindi wao dhidi ya klabu ya Liverpool kesho ndio utawafanya kuonekana wako makini na wanahitaji ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.

Kikosi cha Manchester United kitakua na kibarua kigumu kesho katika dimba la Anfield dhidi ya klabu ya Liverpool, Beki Luke Shaw anautazamia mchezo huo kama taswira ya wao kwenda kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu kama watafanikiwa kupata matokeo.ShawKlabu ya Manchester United wanaonekana kuwinda mataji manne mpaka sasa ndani ya msimu mmoja, Kwani mpaka sasa wameshashinda taji moja la Carabao Cup huku wakiwepo kwenye mataji mengine matatu ambayo ni kombe la ligi kuu ya Uingereza, Fa Cup, pamoja na michuano ya Uefa Europa League na kwa mwenendo wa klabu hiyo mpaka sasa inaonekana wanaweza kufanya jambo lolote.

Beki Luke Shaw akaiuzungumzia mchezo wao dhidi ya Liverpool anasema kama United inataka ubingwa kweli inahitaji kwenda kushinda michezo kama hii, Wakati huohuo anatambua mchezo huo utakua mgumu vilevile Man United haijafanikiwa kushinda Anfield tangu mwaka 2016.ShawLuke Shaw anasema kua wao wanaweza kuleta mwanzo mpya klabuni hapo licha ya miaka kadhaa migumu iliyopita ndani ya klabu hiyo, Beki huyo anasema ni wakati wa kutengeneza zama mpya wakiwa na meneja mpya, wachezaji wapya, timu mpya, pia akiona ni mwanzo mzurio katika mwelekeo wanaoutaka.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa