Meneja Ronald Koeman anaonekana kutokuwa na mipango mikubwa na Riqui Puig na Samuel Umtiti.
Raisi wa Barcelona, Joan Laporta, anatamani wachezaji hawa watumike zaidi kwenye kikosi cha Barcelona katika mwanzo wa kampeni ya ligi pale La Liga.

Nyota hawa wawili hawakupokea ofa ambazo zilikubaliwa na maobosi wa Barcelona wakati wa msimu wa uhamisho, kuwepo kwaop Barcelona kulitarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko klabuni hapo.

Hata hivyo, Puig na Umtiti, wote hawakupata mda wa kucheza mwezi Agosti wakati wa maandalizi ya msimu mpya, ikiwa ni ishara kuwa Meneja Koeman huenda hana mipango mikubwa na wachezaji hawa kwenye kikosi chake cha kwanza.
Lakini taarifa zinasema kuwa Raisi, Laporta ana imani kubwa na wachezaji hawa ikiwa watatumiwa vizuri.
Kwa mujibu wa The Marca, Laporta anataka meneja Koeman awatumie vizuri Puig na Samuel Umtiti kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


