Kutoka Bambali: Ukubwa wa Ndoto kwa Mane

Ni nani asiyemjua Mane? Bila shaka mmeitika “hakuna”. Kama yupo basi huyo hahusiki na hiki tunachojadili hapa! Nyaraka muhimu kama pasi ya kusafiria, kitambulisho cha kuzaliwa na vingine kama hivyo vinamtamua kama Sadio Mané. Fulana ya Liverpool yenye jezi namba 10 inamtambulisha kama Mané. Na sisi tukalipokea hilo la kwenye fulana, labda ni kwa sababu ya uvivu tu Wa kulitamka jina lote ama kwa sababu ya urahisi wa kuliacha lile la kwanza, pengine ni kwa sababu ya yote hayo na mengineyo.

Kuna tukio kubwa lilitokea Siku ya jumatatu ya December 2 mwaka 2019 katika ukumbi maarufu wa Théâtre du Châtelet uliopo ndani ya jiji mashuhuri la Paris. Ni tukio ambalo, pamoja na kwamba kuna mengine mengi ya aina yake yanekuwa yakifanyika hapo kabla, hili la usiku ule pale Paris lilikuwa na upekee wa aina yake. Lina kila sababh ya kubaki katika kumbukumbu za kila mpenda soka. Siku ile kulifanyika sherehe za utoaji wa tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia ‘Ballon d’Or” na upekee wa siku hii kwa siku zingine kama hizo ni ule ukweli kwamba yule aliyechukua tuzo hiyo mwaka huo aliichukua kwa mara ya sita na kumfanya kuwa mtu wa kwanza kufanya hivyo! Lionel Messi alijibebea tuzo yake kisha mambo mengine yakaendelea.

Moja kati ya matukio mengi yaliyotokea siku ile ni pale ambapo fundi huyo wa soka alipopata nafasi ya kuzungumza kidogo kuhusu ushindi wake huo. “Ni aibu kuona Mane ameshika nafasi ya nne. Nafikiri kulikuwa na wachezaji wengi wazuri katika kinyang’anyiro hiki hivyo kupelekea ugumu katika kuchagua mshindi. Lakini nimemchagua Mane kwa sababu ndiyo mchezaji ninayevutiwa nae”

Kauli hiyo ya Messi haikuwashtua watu lakini kidogo iliwashangaza. Kwa tafsiri ya haraka haraka ni kwa Messi alitegemea kuona kama sio yeye basi Mane anashinda tuzo hiyo na siyo mchezaji mwingine yeyote.

Mane mpaka sasa anakunja kibindoni mshahara unaokadiriwa kuwa zaidi shilingi 300,000,000 za kitanzania kwa wiki! Ni mchezaji wa kutegemewa pale Anfield, hali ni hiyo hiyo hata katika timu yake ya taifa. Anaheshimika na kutegemewa pia.

Heshima, utajiri na maisha ya kifahari anayoishi hakuzaliwa navyo Mane. Ilimbidi kuhangaika sana ili avipate hivyo vyote.

Mane ni ushahidi unaoishi wa ile kauli maarufu ya ‘Kuzaliwa maskini siyo kosa lako bali kufa maskini’.

Tangu akiwa mvulana mdogo Mane alikuwa na ndoto ya kuja kuchezea ligi kuu ya Uingereza ambayo alikua akiiona tu kupitia luninga za majirani zao. Umbali wa Kilomita zaidi ya 4,368 kutoka Senegal mpaka Uingereza, hali yake ya kukosa elimu ya darasani sababu ya umaskini mkubwa uliofanya wazazi wake washindwe hata kumlipia ada ya shule kamwe havikuwahi kuwa sababu ya Mane kuikatisha ndoto yake hiyo.

Mane amekua bila baba, mzee alipoteza maisha akiwa bado kijana mdogo na hapo ndoto zake za kuipata elimu ya darasani zikakoka kabisa. Ilimbidi kulelewa na mjomba wake, huko nako maisha hayakuwa vizuri. Kukosa msosi ilikuwa kawaida tu, dogo hakukatishwa tamaa na hayo, aliendelea kulisakata kabumbu la mtaani kama kawa. waliamini

Huko kijijini Bambali alikokulia Mane walimtambua kama kijana mtundu tu anaeweza kuucheza mpira, Walimtambua tu kama mchezaji bora wa Bambali, hakuna aliyefikiria au kuota kwamba atakuja kuwa mchezaji bora Afrika, tena mchezaji tegemeo wa timu kubwa kama Liverpool.

Labda Messi alisikia kwamba kijijini Kwao Mane walimuita ‘Ballonbuwa’ (mchawi wa soka) akaona kuwa anastahili Ballon D’or. Sababu haiwezi kuwa hiyo,  Messi anaujua uwezo wa Mane. Pengine naye angekuwa mzaliwa wa Bambali angekubali kuwa Mane ni Ballonbuwa kweli.

Umbali mrefu kutoka Senegal mpaka Uingereza na umaskini uliokithiri havikuwa vikwazo pekee kwa Mane kutimiza ndoto yake,  hata familia yake pia haikuamini katika mchezo huo. Wao walikuwa watu wa dini sana, na wasingetaka mtoto wao apotelee katika soka. Au aendelee kupoteza muda na nguvu zake kwa ndoto ambazo kamwe haziwezi kutimia. Walitaka hizo nguvu azielekeze katika kilimo.

Pale ndoto ndoto za kijana huyo zilupoonekana kuwa kubwa na zisizoweza kuziliwa kirahisi ikambidi tu mjomba anyoonye mikono juu kusalimu amri na kuamua kumsaidia kutimiza ndoto hizo. Wanakijiji nao hawakuwa mbali katika kumpa ‘sapoti’ ballonbuwa  wao wakamchangia kiasi cha pesa ili awese kusafiri kwenda mjini Dakar akazitimize hizo ndoto zake. Huo ukawa mwanzo wa faraja kwa Mane, ukawa pia mwanzo wa mwisho wa mateso yake. Jitihada zake huko Dakar zikampeleka klabu ya Metz Ufaransa. Hilo likawa tundu lake la kutokea, Mane akaingia dunia ya wachezaji bora wa kandanda duniani. Kisha mimi na wewe tukamtambua, Messi na wachezaji wengine wakubwa wakamheshimu!

19 Komentara

    Moja kati ya mifano mikubwa sana ya Kuigwa na waafrika

    Jibu

    Mane namkubali sana

    Jibu

    Hana tupa fundisho kwny kutafut hakuhtaj kukata tamaaa Asante meridian kwa habar Moto motao

    Jibu

    Kapiga mafanikio sana #meridianbettz

    Jibu

    Mane mpambanaj sn

    Jibu

    Jamaa yuko vzur sana mane

    Jibu

    Jamaa mkali

    Jibu

    mane mtu mbaya

    Jibu

    MAne mpambanaji sana

    Jibu

    Yupo juuu

    Jibu

    Mane namkubali sana

    Jibu

    Yupo vizur

    Jibu

    Mchezaji bora kwa sas kutokea Liverpool….ongeza bidii #Meridianbettz

    Jibu

    Mane mtu mbaya

    Jibu

    Mmoja wachezaji 10 bora dunian. Fundi sadio mane kipenzi cha wasegenal & liverpool #meridianbettz

    Jibu

    Fundi wa liver.

    Jibu

    Respect kwake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.