Kylian Mbappe hivi karibuni amesaini mkataba mpya na klabu ya PSG, ambapo awali alipanga kuondoka klabu hiyo baada ya mkataba wake kuisha majira ya kiangazi.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa sasa inasemekana kuwa ana nguvu kubwa ndani ya klabu hiyo, na anaweza kuishawishi klabu hiyo kutaka kuungana na mchezaji mwenzie wa zamani ambaye alicheza na kwenye klabu ya Monaco.

Kylian Mbappe

Fabinho aliwai kucheza na nyota huyo wa klabu ya PSG Kylian Mbappe, na kuna taarifa kuwa mchezaji huo wa kimataifa wa Ufaransa anataka kuungana na Fabinho ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Liverpool.

Kumshawishi nyota huyo wa Liverpool kwa sasa inaweza kuwa kazi ngumu, kwani kwa sasa ni moja ya viungo wa ulinzi bora duniani na ni sehemu ya kiungo tegemezi wa klabu Liverpool kwa sasa.

Ingawa klabu ya PSG imekuwa ikifanya maboresho ya kikosi chao hasa hasa kwenye nafasi za ushambuliaji na nafasi za ulinzi zaidi kuliko nafasi za viungo zaidi, huku nafasi ya kiungo wa ukabaji akicheza zaidi Marquinhos.

Ikiwa Fabinho atafanikiwa kusajiriwa na klabu ya PSG basi atakwenda kuziba nafasi ya kiungo mkabaji kwenye klabu hiyo.

Kwa sasa kuna taarifa kuwa Kylian Mbappe anajaribu kushawishi bodi ya klabu hiyo kuweza kuimarisha nafasi ya kiungo ili kuboresha eneo la katikati ili kusaidia kusukuma mpira kuwafikia zaidi.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa