Mchezaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema amekutwa na hatia ya kula njama ya kutaka kupata pesa kwa mchezaji mwenzie ili asisambaze video ya ngono, ambapo kesi ilianza mwaka 2015 na sasa imekamilika na kukutwa na hatia ambapo amehukumiwa kwenda jela kwa miezi la 12 na faini ya  €75,000.

Mahakama ya Versailles, imemkuta na hatia ya kushiriki kula njama ya kupata pesa kwa mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Valbuena ili wasisambaze video zake za ngono.

Karim Benzema

Karim Benzema ni moja ya watu watano ambao walikula njama hiyo, ambao wameshitakiwa kwa kutaka kupata pesa kutoka mchezaji huyo ili wasisambaze video hiyo. Benzema anashutumia kula njama na washitakiwa wengine ili kumpa presha Valbuena dhidi ya video yake ya ngono ambayo ilibiwa kutoka kwenye simu yake.

Mahakama ilisema kwamba Benzema alijihusisha yeye mwenyewe, kwa hila zake mwenyewe na uongo, ili kumshawishi mchezaji mwenzie kuweza kulipa kiasi cha fedha kilichokuwa kinahitaji ili wasiweze kumchafua.

Pia alisema kwenye maelezo yake, “hakuwa na huruma dhidi ya Valbuena, kama alivyodai, lakini badala yake alikuwa upande wa kumkandamiza”

Karim Benzema kesi ilimfanya asicheze timu yake ya taifa Ufaransa kwa muda wa miaka mitano, lakini baada kuonyesha kiwango cha kuvutia amefanikiwa tena kuitwa kwenye timu hiyo, huku Valbuena mpaka leo hajafanikiwa kuitwa tena kwenye timu hiyo.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa