Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe anatumai kwamba Aurelien Tchouameni atajiunga naye katika klabu ya Paris Saint-Germain licha ya mchezaji huyo wa Ufaransa kuwa kwenye windo la Real Madrid.

Mbappe alikubali kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya jiji la Ufaransa siyo sababu ya fedha pekee bali alishawishika kwa kikosi cha PSG kwa msimu ujao.

Na klabu imeweka wazi kwamba kipaumbele chao kwa sasa ni kuimarisha safu ya kiungo na Tchouameni ndiyo yupo mstari wa mbele katika malengo yao.

Sio tu kwamba Tchouameni anapendwa na Luis Campos, ambaye tayari anasimamia mradi huo mpya pamoja na Nasser Al Khelaifi, hata kama bado hajathibitishwa rasmi, lakini Mbappe pia anajua uwezo mkubwa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.

Mbappe na Benzema wote wanajaribu kumshawishi chipukizi huyo kujiunga na klabu zao msimu huu wa joto, swali Je nani atafanikiwa? Acha tusubiri.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa