Katika hali ya kawaida, hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu na vilevile hakuna timu kubwa kuliko shirikisho la soka la mahali husika. La Liga ipo tayari na maisha bila ya Lionel Messi.
Mapema mwezi Agosti, Lionel Messi aliwasilisha maombi yake ya kutaka kuondoka kwenye klabu ya Barcelona. Mchakato ambao uliteka vichwa vya habari duniani kwa muda kufuatia sakata hili kuwa na maelezo mengi kwa kila upande uliohusika.
Japo ombi la Messi halikufanikiwa na aliendelea kubaki Barcelona, La Liga ilishuhudia raisi wa Barca – Josep Maria Bartomeu akijiuzulu baada ya sakata la Messi kuondoka Barcelona kuisha.
Hii haijawashtua La Liga na wametolea mfano baadhi ya wachezaji waliowahi kuondoka kwenye ligi soka nchini Hispania lakini maisha yameendelea bila tatizo lolote na ushindani upo vilevile.

Akizungumza na waandishi wa habari, Raisi wa La Liga – Javier Tebas amenukuliwa akisema “Tungependa Messi abaki lakini Ronaldo na Neymar waliondoka na hatujaona tofauti yoyote mpaka sasa. Tupo tayari.
“Inaonekana timu pekee kwenye Premier League ambayo ilisemekana inamtaka Messi ni Manchester City, hawa wanafanya kazi nje ya utaratibu. Sio mimi tu ninayesema hili.
“Sina uoga wowote dhidi yao. Mara kadhaa nimewakosoa kwa wanachokifanya. Kukirudia tena kwa mara nyingine haina tofauti yeyote. City hawajaathirika na COVID au gonjwa lolote au changamoto yoyote kwa sababu wanamfumo tofauti wa kifedha na ni ngumu kupambana na hilo.”
Je, Messi ataondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu au ataamua kusaini mkataba mpya na Barcelona hasa baada ya Bartomeu kujiuzulu na ujio wa uongozi mpya?
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.



magdalena
kama laliga wameamua bila messi soka aliwezi kuzuirika basi haina tabu maisha ya soka yaendelee tu
Adelta
La liga iko vizuri na inajiamini itazidi kunoga
Mwajumah
Acha maisha ya soka yaendelee na la liga kama kawa kwani Messi yeye nan mpaka akwamishe laliga
Khadija
Leo kazi ipo
Aziza mushi
La liga ipo vizuri .
Angelina
Yuko sahihi
Sadick
Ni kauli ya kishujaa. Maisha yanatakiwa kuendelea bila Messi.
ester jackson
La liga acheni maneno maneno kwani messi ndio amebeba timu au yeye ni mchezaji kama wachezaji wengine mbona mnaleta ushamba au mmeshapewa chenu na Barcelona mnaanza maneno madogo dogo acheni hizo akiamua kuondoka ni yeye mwenyewe na kikosi chake kama ilikuwa hamumtaki si mngemuacha akaondoka mbona mlimuwekaa vikwanzo ni kwa sababu mlikuwa munamuhitaji hasaivi mnaaza kutupigia kelele.
Fatina mfingi
La liga pamenoga!
Samira
La liga nao wamuache messi amalizane na Barcelona bila maneno maneno wamuache akamalizie soka lake anapotamani kumalizia
Gabriel
wamuache akamalizie soka lake anapotamani kumalizia
Carolyn
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu
Rahma
La liga ipo vizuli
Elika
La liga haishindwi bila mess
zeiyana
Barcelona kama wana mtaka messi waendelee nae na bishara wamuongezee dau tu pesa ndio kila kitu
Devotha
Mmmh laliga nao wanamaneno kama bongo tu
Hopemwaikuka
Jamani kwan Messi kawakosea nn mbona hvyo
Antony Luseno
Kauli nzuri sana alilosema na inawezekana kabisa
Sauda
La liga mambo ni moto.
Nasra
Kumekucha huko laliga
Fatuma kasomo
Mambo yamepamba moto
Povel
Ni kauli ya kishujaa tu ila ukwl ni mwamba La liga bila messi haina mvuto na vile vile wanapotezah pesa nyng Sana kutokuwepo messi ndani ya la liga
aisha
Mmmmmhh naona sio powa kabisa
Theonestina
Duuuh
Sabrina
La Liga bila messi inawezekana
felister
Yuko sahihi
Lydia Emmanuel Magoti
Mbona hili gumzo tena wamuache aende anapo taka kwenda akamalizie soka lake semu anapo pataka Messi kasha choka kusalia hapo Barcelona wamuache ende tuu
Saupha mohamed
La liga IPO vizuri
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif meridianbet