Kocha wa klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza Frank Lampard anaamini mshambuliaji wa timu Dominic Calvert Lewin anaweza kuitwa kwenye kikosi cha mwisho cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachokwenda nchini Qatar kushiriki kombe la dunia.
Huku Calvert Lewin akiwa anatokea benchi bado mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney ana kiwango kizuri kwasasa lakini kocha hajamkatia tamaa mshambuliaji wake huyo.
“Tunapaswa kua makini na Dominic akirejea,Tukihakikisha tunamleta taratibu lakini haraka iwezekavyo” Alizungumza Lampard na waandishi wa habari.
Domic Cavert Lewin alikua na kiwango bora sana chini ya mwalimu Carlo Anchelotti wakati akiwa Everton lakini hali ilibadilika alipopata majeraha na kuanzia hapo hakuwahi kurudi kwenye ubora wake tena amekua mchezaji wa kuumia mara kwa mara.
Lakini Lampard anaamini mchezaji huyu anaweza kufanya vizuri hizi dakika za mwisho na kuitwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakochoshiriki kombe la dunia.

