Leicester City Mambo Bado ni Magumu.

Leicester City mambo yanaonekana bado kua magumu kwa upande wao baada ya kupokea kipigo cha goli tano kwa mbili dhidi ya Brighton Hove Albion.

Katika mchezo huo uliopigwa mapema kabisa katika dimba la The American Express Community Stadium ni Leicester waliopata bao la kuongoza kupitia kwa Kelechi Ihenacho kabla ya vijana wa Graham Potter baada ya beki wa Leicester kujifunga na kuufanya mchezo kua sare dakika mbele Brighton wanapata bao la pili kupitia kwa kiungo Caicedo kabla ya Patson Daka kusawazisha na mchezo huo kwenda mapumziko kwa sare ya goli mbili kwa mbili.

leicester cityKipindi cha pili ndo hapo vijana wa Brendan Rodgers walionekana kuelemewa na kufungwa goli tatu kupitia Leandro Trossard pamoja na Mcallister aliefunga magoli mawili na kufanya idadi kua tano kwa mbili na mchezo kumalizika namna hiyo.

Mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Uingereza wanabaki mkiani mwa ligi hiyo baada ya kukusanya alama moja kwenye michezo sita waliyoingia uwanjani baada ya kupoteza michezo mitano na kupata suluhu mchezo mmoja.

Hii si dalili nzuri kwa klabu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Kingpower kwani kupoteza michezo mitano mfululizo katika ligi kuu ya Uingereza ni kujiweka katika mazingira magumu sana.

Acha ujumbe