Lewandowski ni Kama Ronaldo na Messi

Tunapozungumzia mafanikio katika soka wapo wale ambao huwa na bahati ya kukaa sana kwenye vinywa vya mashabiki wa soka kwa kipindi kirefu lakini pia wapo wale ambao wao kwa upande wao huzunguziwa baada ya kufanya tukio fulani kubwa ambalo ni sehemu ya historia na ambalo linaendana na wawili hao.

Nyota wa klabu ya Bayern Munich mara nyingi amekuwa akifanya mambo makubwa ambayo kwa hakika ni sawa kabisa na yale yanayofanywa na miamba wawili wa soka kwenye karne hii Messi na Ronaldo. Nyota huyo amekuwa muhimili mkubwa sana ndani ya kikosi cha Bayern kitokana na uwezo wake.

Inapozungumziwa suala la magoli, nyota huyo anafunga kwa kiwango cha pekee sana kitu ambacho siyo cha kubeza. Ameweza kuibuka kinara wa kufunga mara nyingi sana katika ligi hiyo ya Ujerumani na kunyakua kiatu cha ufungaji bora. Mbali na hilo kwa matokeo mengi ambayo Bayern wamekuwa wakiyapata amehusika kwa nafasi kubwa sana.

Mafanikio mengine ambayo hadi sasa anayo lakini hayazungumziwi sana ni ndani ya msimu huu ambapo hadi sasa ni nyota wachache sana walioweza kuwa na rekodi kama yake. Katika mechi 11 ambazo amecheza tayari ndani ya msimu huu ana rekodi ya kuweza kufunga katika kila mechi aliyoingia uwanjani.

Ni aina fulani ya watu ambao wanajua uelekeo wa goli na timu inahitaji kitu gani ili kuweza kupata ushindi na kusonga mbele. Kufunga mfululizo kiasi hicho sio jambo rahisi kabisa hasa katika mechi za ushindani ambao kwa sasa umeweza kugeuka kuwa nguvu kubwa sana na kila mmoja hataki kuonekana mzembe mbele ya mwenzake.

Werner ambaye alikuwa akiangaliwa kwamba angekuwa mbadala wa nyota huyo ndani ya kikosi hicho anaweza kumzungumzia Lewandowski kama mtu ambaye kwa soka la sasa ananyimwa tu hadhi ya kuwa sawa na wawili hao japo kwa hakika uwezo wake ni mkubwa na anajua nini anachokufanya akiwa na mpira.

Kwa msimu huu Messi pekee ndiye anayemzidi idadi ya magoli nyota huyo mbali na hapo wengine wanafuatia baada yake. Hiyo ni nafasi kubwa sana kwake na kwa umri ambao bado anaonekana kuweza kuwa nyuma ya wawili hao. Japo huenda aina ya ligi anayocheza haimpi nafasi kubwa sana ya kuweza kuuza kama wawili hao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.