Nyota wa Wolveshampton, Raul Jimenez aliripotiwa kuwa yuko mbioni kusajiliwa na moja ya klabu kati ya Arsenal na Manchester United. Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa siku chache zilizopita ni kuwa Mashetani Wekundu na Washika Bunduki wote walikuwa wameonesha nia ya kuinasa saini ya staa huyu.
Hata hivyo, habari mpya zinataja kuwa nyota huyu amezitema habari za yeye kutaka kuondoka klabuni hapo baada ya kuhusishwa na klabu hizo mbili za EPL.
Jimenez amabaye kwa sasa ana umri wa miaka 28, ameifungia Wolves magoli 39 tangu alipojiunga na klabu hiyo. Awali alijiunga kwa mkopo akitokea Benifica kisha Wolves walimsajili kwa mkataba wa kudumu kwa ada ya paundi milioni 30 na ameanza vyema kwa kuwachapia magoli mengi.

Baada ya kusaini mkataba wake wa kudumu Raul Jimenez hana nia ya kuondoka klabuni hapo, staa huyu aliamua kuzungumzia suala hili kwenye mtandao wa Facebook katika maswali na majibu na kusisitiza kuwa kwa sasa ana mkataba ambao unamlazimu yeye kuendelea kuwepo klabuni hapo hadi mwaka 2023.
Baadhi ya minongono ilitaja staa huyu ataweza kusalia klabuni hapo ikiwa watafanikiwa kufuzu kuingia kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya. Jimenez amekanusha na kuweka wazi kuwa si lazima wafuzu kuingia ligi ya mabingwa ndipo yeye aweze kusalia klabuni hapo. Amesisitiza kuwa kwa sasa ana furaha kuwa klabuni hapo na ana imani kuwa kikosi kizima kinafuraha kama yeye.
“Sio kwamba ni lazima tufuzu Ligi ya Mabingwa ili kubakia. Niko poa hapa, nina furaha na Wolves, kufanya vitu muhimu mimi pamoja na wana team wenzangu. Tumejitahidi sana kujaribu tangia mwanzo wa msimu uliopita. Tumefanikiwa kuingia Ligi ya Europa na sasa tunapambana kuingia Ligi ya Mabingwa.” -Raul Jimenez
Licha ya ukubwa wa majina ya Arsenal na Man United, ukilinganisha na mwajiri wake wa sasa, Raul Jimenez anajiona kuendelea kuwepo Wolves kwa mda mrefu zaidi.


Furahav
Aende tu man u