Kunako soka la Ufaransa – Ligue 1, mchezo kati ya PSG na Marseille ulihitimishwa kwa vurugu zilizopelekea kadi 5 nyekundu ndani ya dakika za nyongeza.
Mchezaji nyota wa PSG – Neymar Jr, Parades, Kurzawa pamoja na Amavi na Benedetto wa Marseille walipewa kadi nyekundu kwa kuhusika na vurugu zinazosemekana chanzo ni ubaguzi wa rangi.
Mchezo ambao ulimalizika kwa PSG kupoteza kwa goli 1-0 ikiwa ni mara yao ya kwanza kuanza msimu kwa kupoteza michezo miwili mfululizo tangu mwaka 1984-85, kulizuka taharuki na wachezaji kushikana mashati zikiwa zimesalia dakika 2 mchezo kumalizika.

Ilimbidi muamuzi wa kati kuangalia VAR na kujiridhisha kuwa ni makosa kwa wachezaji hao na kuamua kuwapatia kadi nyekundu wote watano kwa kuhusika kwenye kitendo hicho.
Baada ya mchezo huo, Neymar aliweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema, “ninachojutia ni kutokumpiga usoni Alvaro Gonzalez.”
Gonzalez nae akajibu kwa kusema, “hakuna nafasi ya ubaguzi”. Kocha wa Marseille – Andre Villas Boas amenukuliwa akisema, “hakuna nafasi ya ubaguzi kwenye mpira, lakini sidhani kama hicho ndo kilichotokea, tunapaswa kuliangalia hilo.”
Je, PSG wataendeleza ubabe wao kwenye Ligue 1 msimu huu?
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Ester jackson
Huu baguzi sio mzuri kabisa kwa halii inapoteza ladha ya mpira kwa ujumla
Latifa juma mohamed
hakuna nafasi ya ubaguzi kwenye mpira, vema kwa wote kupewa kadi nyekundu
Mwanahamisi
Ubaguzi ni Jambo baya sana
warda
Jamani mbona Wanaanza kujipanikisha tena#Meridianbettz
Flomena
Ubaguzi sio mzuri mahali popote pale yani
Zeiyana
Neymar kama akiendelea hivi hatapoteza mashabiki wake na ustar wake pia ukingalia juzi tu ametoka kupewa dili na kampuni ya puma kuitangaza kampouni yao
Elika
Mwanzo mbaya huo
Asia Abdy
Duh sio poa
Caroline
Duh pole yakee
Adelta
Ubaguzi sio mzuri pole yake@meridianbettz
Lydia Emmanuel Magoti
Duu noma Sana
Fatina mfigi
Mmh majanga!!
felister
duh wameanza vibaya
Janeflora malisa
Dah
rama
sawa kabisa tena ikobidi wafungiwe hao
Fatuma kasomo
Mh noma
Rose kapinga
Mambo ya kizamani hayo sasa ivi kila mtu hana haki sawa
Tatu
Hivi kwanini huu ubaguzi wa rangi wanaupeleka hadi kwenye mpira
Salma ngende
Hii mbaya sana
Hopemwaikuka
Sio poa kabsaa
Hidaya
Ubaguzi wa nini sasa jamani kwenye mpira
Theonestina
Sio poa
Amiri Kayera
Hii naon imevunja record
Gabriel
ubaguzi wa rangi wanaupeleka hadi kwenye mpira
Sabrina
Waache ubaguzi wa rangi watapasuka Neymar ataki masihara
Saupha mohamed
Mmmh si jambo zuri
Genia Sikaluzwe
Mmmh noma
Theckla
Watu hawaelimiki
Dorophina
Ubaguzi wa rangi ushakuwa Ni tatizo kubwa kama linaingia mpaka kwa watechazi mpira utakuwa hauna radha kabisa
Sauda
Ubaguzi siyo poa
magdalena
huu ubaguzi ukiendelea itakuwa mbaya sana maana watu wenye ngozi nyeusi itafikia hatua watagoma kucheza katika mechi za watu wenye ngozi nyeupe
Nasra
Sio poa kabisa
Neema
Ubaguzi sio poa
Povel
Duh noma sana
Samiah
Sio poa
David Pere
hakuna nafasi ya ubaguzi kwenye mpira, vema kwa wote kupewa kadi nyekundu