Hayawi hayawi, sasa yamekuwa. US Open 2020 imemalizika kwa namna ya kipekee, michezo ya fainali ilikuwa na burudani ya aina yake. Thiem na Osaka mabingwa wapya wa Mashindano haya.
Kwa upande wa wanaume, Thiem alikuwa akichuana na Zverev katika fainali ya Grand Slam mwaka huu. Mchezo ambao Zverev alikuwa na nafasi kubwa ya kuutwaa ubingwa mwaka huu, alianza vyema ila alishindwa kumalizia ‘mkia’ wahenga wanasema.
Thiem alipata ushindi akitokea nyuma kwa seti mbili na kuibuka kidedea kwa matokeo ya 2-6 4-6 6-4 6-3 7-6 (8-6) dhidi ya Zverev ambaye pia ni rafiki yake tangu utotoni.

Hii ilikuwa ni fainali ya kwanza kwa Zverev katika hatua ya Grand Slam lakini ilikuwa ni fainali ya 3 kwa Thiem kwenye Mashindano ya US Open baada ya kulikosa kombe hili katika fainali mbili alizocheza.
“Natamani tungekuwa na washindi wawili leo, wote tulistahili ushindi huu.” Thiem alimwambia Zverev.
Mwanadada Naomi Osaka alikuwa na wakati maridhawa alipokutana na gwiji Azarenka katika Fainali ya US Open 2020.
Osaka ameendelea kuonesha kiwango chake kinachozidi kukua siku baada ya siku. Hili ni taji lake la 3 la Grand Slam, 2018 alibeba kombe la US Open na 2019 akachukua Australian Open.

Osaka alishinda kwa jumla ya seti 1-6 6-3 6-3 na kubeba taji lake la 2 la US Open. Baada ya mchezo huu, Osaka alimtania Azarenka kwa kusema, ” Sitaki kucheza na wewe tena kwenye fainali nyingine yeyote,sijaufurahia mchezo, ulikuwa mgumu sana kwangu.
“Hili limekuwa tukio la kunivutia kwani nimekuwa nikikuona tu ukicheza kwenye kiwanja hiki wakati nikiwa mdogo, nimejifunza vingi, asante sana.”
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Ester jackson
Huyu Naomi hatari kabisa ubigwa yeye utaji namba moja yeye jamani kunawata wananeema sana hongeza zake
Elika
Ushindi ni haki yao.hivyo wanastahili pongezi kwa kazi nzur
Latifa juma mohamed
Osaka ameendelea kuonesha kiwango chake kinachozidi kukua siku baada ya siku. Hili ni taji lake la 3 la Grand Slam, 2018 alibeba kombe la US Open na 2019 akachukua Australian Open, so nice congr NAOMI OSAKA!!
warda
Osaka amefurahia sana huu Ushindi#Meridianbettz
Zeiyana
Zverev na azarenka wasivunjike moyo sana kwani hadi kufikia fainali juudi kubwa wamefanya kikubwa wajopange tu michezo bado hipo na hinaendelea
Asia Abdy
Pongez kwao
Caroline
Hongera Sana Thiem na Osaka
Lydia Emmanuel Magoti
Haki yaho kupata ushindi wanapambana sana
felister
wamestahili ushindi ongera zao
rama
safiii
Rose kapinga
Pongezi kwao,kazi nzuri wamefanya!!!
Tatu
Kazi nzuri aliyoifanya Naomi apewe pongezi kwa sasa naona hana mpizani
Theonestina
Pongezi ziende kwao
Sabrina
Wooh hongera zao
Tumaini kasalile
Walk vzuri hongera kwao
Sauda
Osaka amefurahi sana
magdalena
pongezi nyingi sna kwao juhudi zao ndo zimewafikisha apo walipo
Samiah
SAfi
David Pere
Huyu Naomi hatari kabisa ubigwa yeye utaji namba moja yeye jamani kunawata wananeema sana hongeza zake