Licha ya kuwa amebakiza miezi michache mkataba wake na Manchester United kumalizika, mpango wa Newcastle United kwa Jesse Lingard, umegonga mwamba.
Newcastle wanahaha sokoni kutafuta wachezaji wa kuimarisha kikosi chao kuelekea mwishoni mwa msimu. Wameshawasajili Chris Wood na Kieran Trippier na sasa, waligonga milango ya Man United na kupeleka ofa ya kumsajili Lingard kwa mkopo wa miezi 6.
Kama kawaida yao, viongozi wa Man United hawana njaa ya pesa. Wana mipango na mikakati yao kwa kila mchezaji kwa nafasi yake. Kimsingi, ofa ya The Magpies imetupiliwa mbali.
Sababu kubwa ikiwa ni, endapo Newcastle watamsajili kwa mkopo, hii inamaanisha kuwa, safari ya Jesse ndani ya United itakua imeisha rasmi kwani anamaliza mkataba msimu huu.
Kwa hali ilivyo, Manchester United itawauza wachezaji wote wanaomaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu kama timu inayomtaka mchezaji itamchukua kwa mkataba wa moja kwa moja, sio mkopo.
Paul Pogba, Jesse Lingard, Edinson Cavani na Juan Mata ni miongoni mwa wachezaji wanaomaliza mikataba mwishoni mwa msimu huu.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA