Andy Murray Atolewa Australian Open 2022.

Amahakika, ng’ombe wa masikini hazai. Licha ya kuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na majeruhi, kurejea kwa Andy Murray kumeishia mzunguko wa pili kule Melbourne.

Murray amerejea kwenye mashindano ya Grand Slam mwaka huu kunako Australian Open baada ya kuwa nje ya uwanja toka alipocheza mashindano haya mwaka 2019. Majeruhi ya paja, yalimfanya ahisi ndio mwisho wake wa kucheza tenesi lakini, haikuwa hivyo, alipona na akarejea tena uwanjani mwaka huu kwenye mashindano yaleyale – Australian Open.

Mchezo dhidi ya Taro Daniel (namba 120 kwa ubora duniani[wanaume]) umekuwa ndio mwisho wa Andy Murray kwenye mashindano ya mwaka huu, 2022. Hakika, Murray alikuwa na wakati mbaya uwanjani ambapo, ameshuhudia akipigwa kwa matokeo ya seti 6-4 6-4 6-4.

Hii ni mara ya kwanza kwa Murray kupoteza mchezo wa Grand Slam dhidi ya mchezaji anayeshika kiwango cha chini kwa ubora kama Daniel.

Kutolewa kwa Murray, kunamfanya Dan Evans kuwa ndiye muingereza pekee (mwanaume) aliyebaki kwenye mashindano ya Australian Open, 2022.

Stefano Tsitsipas

Pamoja na Daniel, Stefano Tsitsipas na Andrey Rublev pia wamefuzu hatua ya tatu. Tsitsipas amefunga Sebastian Baez kwa matokeo ya seti 7-6 (7-1) 6-7 (5-7) 6-3 6-4 kwenye mchezo uliochukua masaa 3 na dakika 22. Rublev amemfunga Ricardas Berankis kwa seti  6-4 6-2 6-0.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe