Liverpool: Tunaweza Bila Salah na Mane?

Wakati soka barani Ulaya likiendelea, AFCON nayo inaendelea mwezi huu. Liverpool wanaanza kuipata ladha halisi bila ya Mo Salah na Sadio Mane.

Salah, Mane na Keita ni wachezaji watatu wanaokosekana kwenye kikosi cha Liverpool kutokana na ushiriki wao kwenye mashindano ya AFCON mwezi huu.

Ni dhahiri, kukosekana kwa wachezaji hawa, kumepunguza makali ya The Reds ambao mchezo dhidi ya Arsenal ulionesha kile kinachokosekana kwenye timu hiyo.

Licha ya kutawala mchezo kwa 80%, wakiwa Anfield, The Reds walifanikiwa kupiga mkwaju mmoja tu uliolenga goli. Pamoja na Arsenal kupata kadi nyekundu na kucheza muda mrefu wakiwa pungufu, vijana wa Klopp hawakuwa na makali yeyote mbele ya ukuta wa Mikel Arteta.

Salah (Misri), Mane (Senegal) na Keita (Guinea Bissau)

Klopp amekiri,

Hali halisi inaonekana. Hawapo hapa lakini ni wachezaji wenye viwango vya dunia. Tunawakumbuka? Ndio, lakini sio kuhusu nani hayupo ni suala la tunaboresha vipi kwenda mbele.

Salah na Mane watakosekana kwenye kikosi cha Jurgen Klopp mpaka Februari 6, 2022 endapo timu zao zitafanikiwa kufika fainali ya AFCON.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe