Staa mpya wa Atletico Madrid, Ademola Lookman, ameanza kwa moto maisha yake mapya ndani ya kikosi hicho mara baada ya kujiunga akitokea Atalanta.
Nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria alipewa nafasi ya kuanza katika mchezo wa robo fainali ya Copa del Rey dhidi ya Real Betis, ambapo Atletico iliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Lookman alidumu uwanjani kwa takribani dakika 80 na kuonesha kiwango cha hali ya juu, akihusika moja kwa moja katika mabao mawili. Alifunga bao moja na kutoa pasi ya bao jingine, akithibitisha thamani yake mapema kabisa ndani ya kikosi hicho.
Mwanzo huo mzuri unaashiria kuwa Lookman anaweza kuwa silaha muhimu kwa Atletico katika harakati zao za kutwaa mataji msimu huu.