Madrid Yaamuru Endrick Arejee Mwishoni Mwa Msimu

Klabu ya Real Madrid imeweka wazi msimamo wake kwa Olimpique Lyon kuhusu mustakabali wa nyota wake chipukizi, Endrick, ikisisitiza kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil lazima arejee Santiago Bernabéu mara tu mkopo wake wa nusu msimu utakapokamilika.

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa Lyon walikuwa wakitamani kurefusha muda wa mkopo wa mshambuliaji huyo kufuatia kiwango chake bora tangu ajiunge nao. Hata hivyo, mabingwa hao wa Hispania wameweka angalizo kuwa hawana mpango wa kuongeza muda wa makubaliano hayo.

Madrid Yaamuru Endrick Arejee Mwishoni Mwa Msimu

Endrick amekuwa katika kiwango cha juu nchini Ufaransa, akifunga mabao matano na kutoa pasi moja ya bao katika michezo mitano pekee aliyocheza akiwa Lyon. Ubora huo ulimfanya atangazwe kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi wa Januari katika klabu hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kiwango hicho cha kuvutia kinaelezwa kuwa ndicho kilichowashawishi Real Madrid kuharakisha mpango wa kumrejesha nyota huyo kijana, wakiamini kuwa yuko tayari kuchukua nafasi katika kikosi chao kikubwa msimu ujao.

Madrid Yaamuru Endrick Arejee Mwishoni Mwa Msimu

Hatua hiyo inaonesha wazi kuwa Madrid wana imani kubwa na maendeleo ya Endrick, wakitaka kuhakikisha wanafaidika na kipaji chake mapema iwezekanavyo badala ya kuendelea kumlea kwa mkopo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.