Mshambuliaji wa klabu ya As Roma Romelu Lukaku hakamati huko kwenye timu yake ya taifa ya Ubelgiji ambapo amekua akifunga anavyojiskia ambapo mpaka sasa ameshafunga mabao manne katika mchezo dhidi ya Azeebaijan.

Lukaku ameshafanikiwa kufunga mabao manne ndani ya dakika 36 za mchezo huo wa kufuzu michuano ya Euro 2024 inayotarajiwa kufanyika nchini Ujerumani.lukakuMshambuliaji huyo anapokua kwenye timu ya taifa ya Ubelgiji mara nyingi anakua ni kama amekamuliwa ndimu, Kwani amekua akifunga mara kwa mara na ndio sababu mpaka sasa mchezaji huyo anaongoza kwa mabao katika timu hiyo.

Mshambuliaji Romelu Lukaku anaendelea kuongeza mabao kwenye kabati lake haswa kwenye timu ya taifa ya Ubelgiji, Huku akiendelea kujisimika kileleni kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa