Kieran Trippier na Jarrod Bowen hawatakuwepo kwenye mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Macedonia Kaskazini.

 

Trippier na Bowen Kuukosa Mchezo Wao Dhidi ya Macedonia

Beki huyo wa kulia wa Newcastle mwenye miaka 33, hatacheza mechi ya leo baada ya kurejea nyumbani kushughulikia suala la kibinafsi.


Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.

Akaunti ya Uingereza kwenye mtandao wa X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, ilisema: “Trippier ameondoka kwenye kambi ya Three Lions, kutokana na suala la kibinafsi na hatasafiri kwenda Macedonia Kaskazini.”

Trippier na Bowen Kuukosa Mchezo Wao Dhidi ya Macedonia

Naye meneja Gareth Southgate alifichua baadaye jana kwamba Bowen pia atakosa mechi baada ya kupata jeraha mazoezini.

Southgate alisema: “Kwa bahati mbaya Jarrod alipata jeraha. Hatufikirii kuwa itakuwa kitu kikubwa lakini hatungehatarisha katika hali hiyo.”

Ni msururu wa hivi punde wa kujiondoa kwenye kikosi cha Gareth Southgate katika kipindi hiki cha kimataifa, wakiwemo mastaa kama Jude Bellingham, Levi Colwill na Lewis Dunk.

Trippier na Bowen Kuukosa Mchezo Wao Dhidi ya Macedonia

Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Three Lions walifanya mazoezi na wachezaji 22 pekee jana kabla ya mchezo wao wa mwisho wa kufuzu mjini Skopje.

Vijana wa Southgate tayari walikuwa wamejihakikishia nafasi yao ya kufuzu kwa fainali huko Ujerumani msimu ujao wa joto kabla ya Ijumaa kushinda 2-0 dhidi ya Malta, huku Trippier akicheza dakika zote 90.

Kuondoka Trippier kunapunguza zaidi chaguo za Southgate katika nafasi ya beki wa pembeni, huku Kyle Walker akiwa ndiye chaguo pekee lililosalia upande wa kulia na hakuna mabeki wa kushoto wanaotambulika waliotajwa kwenye kikosi cha awali.

Trippier na Bowen Kuukosa Mchezo Wao Dhidi ya Macedonia

Fikayo Tomori alianza upande wa kushoto wa safu ya ulinzi dhidi ya Malta kwenye uwanja wa Wembley na anaweza kucheza nafasi hiyo tena dhidi ya Macedonia Kaskazini.

Mchezo unaofuata wa Newcastle ni dhidi ya Chelsea Jumamosi, Novemba 25, huku West Ham wakimenyana na Burnley siku hiyo hiyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa