MADRID wapo katika harakati za kuangalia kwamba kikosi chao kinakuwa na ushindani mkubwa katika msimu ujao bado wapo katika harakati za kusajili majina ambayo yataweza kusaidia kutetea mataji msimu ujao. Hii ni baada ya anguko lao la kipindi kirefu cha msimu uliopita na ukame wa mataji waliopitia.
Wameendelea kutumia pesa zao kama kawaida kwa kuchukua wachezaji ambao tayari wana takwimu kubwa ambazo zinawapa nafasi ya kuonesha makali moja kwa moja. Wameweza kumsajili Mendy kutoka Lyon ambaye ni mlinzi wa kushoto na atawasaidia kwa nafasi kubwa sana.
Mendy amesaini kandarasi ya kuchezea klabu hiyo kwa miaka sita akiwa chini ya utawala wa Perez ambaye hajataka kabisa kurudia makosa ambayo aliyafanya msimu uliopita. Hii ni nafasi pekee kwake kukaa zaidi kwenye nafasi ya kufanya vizuri kwa kiwango cha aina yake kama ambavyo awali walikuwa wakifanya.
Katika sajili hizo ambazo klabu hiyo wamefanya, Hazard amekuwa mchezaji ghali sana ndani ya klabu hiyo. Huku wachezaji wengine kama Miltao na Jovic wataungana na kikosi cha wakongwe wengine ambao tayari wanafanya kazi ya pekee ndani ya Real Madrid.
Gharama zilizotumika kumnasa mchezaji huyo zinakaribia kufikia £50m ambayo kwa kawaida hadi sasa £300m ikiwa ni jumla ya wachezaji wote ambao wamenunuliwa msimu huu. Hii ni dalili chanya ya maandalizi kwa kikosi hicho ambacho kwa nguvu ya usajili unaofanywa msimu huu watakuwa na upinzani wa pekee.
Klabu hizo mbili tayari zimekubaliana juu ya usajili wa mchezaji huyo na klabu yake tayari imethibitisha kwamba nyota huyo ataweza kuondoka ndani ya klabu yao hiyo. Madrid walikuwa kwenye msimu wa mpito ambao kwa nafasi yake ilikuwa ni vigumu sana kukubaliana na matokeo katika mazingira halisi kwa timu kama ile.
Amecheza soka la kuvutia ndani ya klabu ya Lyon akiwa amecheza mechi 30 ndani ya ligi hiyo. Kwa uwezo wake atakuwa na nafasi kubwa ya kuonesha uwezo wake na ataweza kutambulishwa ndani ya klabu yake mpya tarehe 19, Juni na anaonekana kuwa katika nafasi za wachezaji kama Marcelo endapo wakiondoka.


isha
Madrid mmetisha sana
Povel
Habar njema