Griezman Njiapanda

Nyota na mchezaji wa Atletico Madrid ambaye ameweza kusalia kikosini hapo kwa kipindi kirefu sana hadi sasa na kuisaidia timu yake hiyo kufikia hatua ya pekee sana kwenye mataji na michuano mingi barani Ulaya hadi sasa bado hajajua hatma yake ndani ya La Liga kwa msimu ujao.

Nyota huyo amekuwa akihusishwa na kutimka kikosini hapo tangu msimu uliopita na sasa kwa nafasi nyingine anaonekana kabisa kutimkia nje na ligi hiyo mbali na hapo awali aliposema haoni kama angehama ndani ya klabu hiyo ambayo kwake ni kama nyumbani na hakuona kama ana sababu ya kuondoka hapo.

Katika soka kitu kinachokamilisha maisha halisi ya mchezaji ndani ya klabu fulani ni ile hali nzima ya kukaa mahali ambapo kuna ushindani mkubwa sana. Mchezaji anapokaa ndani ya ligi moja na kukosa ule ushindani wa ndani kabisa basi hata hadhi yake kwa wakati fulani huweza kushuka.

Kuna taarifa zilizoanza kumhusisha nyota huyo na klabu ya Ufaransa ambayo imesheheni majina makubwa sana ya kila aina na uwezo wa juu. Wameanza kuangalia kama wataweza kumnasa nyota huyo raia wa Ufaransa. Japo anaendelea kukaa kimya ili kukamilisha michuano anayoshiriki.

Mara ya kwanza alikuwa amehusishwa kujiunga na Barcelona lakini kwake haoni kama atakuwa na nafasi hiyo ya kuendelea kusalia hapo maana ameshakaa ndani ya ligi hiyo kwa kipindi kirefu sana hadi sasa.

Huenda PSG wanaandaa mbadala ili wakiingia sokoni waweze kupata mbadala wa mapema maana nyota wao wawili ambao ni Neymar na Mbappe mmoja wao anaonekana kuwa katika rada za klabu nyingine wakiwemo Madrid, ambao wanafanya biashara za kumaanisha kwa msimu huu wakiwa hawana utani kwa kile wanakifanya.

Pamoja na yote hayo nyota huyo hajataka kabisa kujihusisha na masuala ya usajili kwa sasa akidai kwamba akili yake imeangalia zaidi kwenye michuano ya Euro ambako yupo na kikosi chake cha taifa kwa msimu huu. Umri wake pia unampa nafasi ya kuweza kukaa ndani ya ligi yoyote yenye ushindani.

Maisha yake ya soka yalianzia pale Real Socedad kabla ya kujiunga na Atletico 2014 na safari yake imekuwa ya mafanikio sana kwa kipindi hicho. Amenyanyua mataji mbalimbali yakiwemo yale ya UEFA Europa, UEFA Super Cup na hata Super Copa, hayo ni sehemu ya mafanikio ya nyota huyo ndani ya muda mfupi aliokaa kikosini hapo.

Makala iliyopita
Makala ijayo

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.