Kila kitu huwa na wakati wake ambao kukitambulisha kitu kwa matokeo mazuri au hata yale ambayo hayaridhishi. Wengine hustaafu soka baada ya kutumikia kwa kipindi kirefu kama ilivyokuwa kwa Stanley Matthews aliyecheza soka hadi umri wake wa miaka 50 na wengine kukutana na changamoto kama Marco van Basten aliyecheza soka lake kwa kipindi kifupi sana.
Lakini kwa nafasi fulani tuangalie wale ambao kwa vinywa vyao wameona ni wakati wao wa kupumzika kwenye soka na kupisha vijana kuendeleza karama zao na wao wakiwa tayari wamepata mafanikio na kuweka rekodi zao kubwa ndani ya soka hilo la kulipwa.
Andrea Barzagli, mchezaji mwenye heshima kubwa ndani ya Italia kutokana na mafanikio aliyoyapata ndani ya taifa hilo. Ni miongoni mwa wakongwe wa Juventus ambao waliweza kujenga heshima ya aina yake katika eneo la ulinzi la klabu hiyo hadi leo wanasifika kwa hilo. Kundi lake la mafanikio lina watu kama Chiellini na Leonardo Bonucci.
Robin van Persie, ni aina ya wachezaji wenye mafanikio makubwa sana na wameyaonesha hayo kwa kucheza klabu nyingi kubwa ambazo amezisaidia sana kuibuka na mafanikio ya aina yake. Tangu akiwa Arsenal baadaye Manchester, alikuwa na historia ambayo sio rahisi kufutika. Hata alipojiunga na ligi ya Uholanzi bado amekuwa na mafanikio ya pekee yanayomtambulisha kwenye ulimwengu wa soka.
Xavi, alama ya pekee ya klabu ya Barcelona ambayo haiwezi kupotea. Ameweza kujenga msingi mzuri ndani ya klabu hiyo kuanzia kuipa mataji klabu hiyo hadi hatua nyingine kabisa za kujenga aina ya soka ambalo limekuwa la heshima sana ndani ya jiji la Hispania na ndani ya klabu ya Barcelona. Heshima kubwa ndani ya klabu hiyo inatokana na uwezo wake mkubwa na damu halisi ya kuipigania klabu hiyo.
Petr Cech, mkongwe ndani ya ligi ya Uingereza akiwa na mafanikio katika klabu ambazo amezitumikia kwa kipindi kirefu hiyo ikiwa ni Chelsea pamoja na Arsenal. Amekuwa na msingi wa mafanikio kwenye soka lake tangu ajiunge na klabu hizo ambazo ameweza kuzichezea. Mataji kwake ni vitu ambavyo sio vigeni kwenye historia yake.
Iker Casillas, mlinda mlango ambaye hata baada ya kuondoka Madrid heshima yake bado iliendelea kubaki kama ilivyo. Amefanya makubwa na ya pekee na kikosi hicho na hata alipotua Ufaransa bado alikuwa bora.
Lakini safari ya hawa wote imefika ukingoni.


Povel
Habar njema
devotha
asante kwa habari