Beki wa klabu ya Manchester United Harry Maguire yuko njiani kuelekea klabu ya West Ham baada ya klabu ya Man United na West Ham kufikia makubaliano ya kumuuza beki huyo.

Manchester United wamekubaliana na West Ham kiasi cha zaidi ya paundi milioni 30 kumuuza mchezaji huyo, Huku makubaliano ya maslahi binafsi baina ya mchezaji na klabu ya West Ham yakiwa yamekamilika siku kadhaa nyuma.MaguireHarry Maguire sasa ataondoka klabuni hapo baada ya kudumu kwa takribani misimu minne ndani ya klabu hiyo, Huku akikiongoza kikosi hicho kama nahodha kwa misimu yote aliyoitumikia klabu hiyo kutoka jijini Manchester.

Manchester United wameamua kumuuza beki huyo kuelekea klabu ya West Ham kutokana na kiwango cha mchezaji huyo kushuka, Huku kwasasa wanatafuta mbadala wa mchezaji huyo ambae wamewapa kipaumbele kama Jean Clair Todibo.MaguireManchester United pia wanatarajia kumuuza mchezaji mwingine kwa klabu ya West Ham Scott Mctominay, Lakini bado hawajapokea ofa nyingine baada ya kukataa ya awali ambayo ilikua imemjumisha na Harry Maguire.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa