Mshambuliaji Mpya Man United Apata Majeraha

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Man United Rasmus Hojlund anataarifiwa kupata majeraha ambayo yatapelekea kumueka nje ya uwanja kwa kipindi kifupi.

Rasmus Hojlund inataarifiwa amepata majeraha madogo ambayo yatamfanya kukosa michezo mitatu ya awali ya klabu hiyo, Huku akitarajiwa kurejea katika mchezo kati ya Man United na Arsenal.man unitedMshambuliaji huyo ameshaanza mazoezi klabuni hapo na ameonekana akifanya mazoezi ya peke yake hiyo ikithibitisha kua anaandamwa na majeraha lakini taarifa zinaeleza sio majeraha ambayo yatamueka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Mshambuliaji Hojlund ambaye amejiunga na klabu hiyo kutoka Atalanta ya nchini Italia ambapo wengi wanatarajia makubwa kutoka kwa mchezaji, Kwani klabu hiyo ilikua inahitaji mshambuliaji wa katikati kwa muda mrefu.man unitedNi wazi klabu ya Man United itatumia safu yake ya ushambuliaji ya msimu uliomalizika kabla ya Hojlund kurejea uwanjani, Huku Marcus Rashford akitarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.