Man United Yamuweka Kando Hojlund Kwajili ya Onana

Klabu ya Man United wamekua kwenye mchakato wa kutafuta mshambuliaji mpya kuelekea msimu ujao lakini wameueka kando kwanza mpango huo kwajili kumalizana na dili la Onana.

Man United walikua wanamfukuzia Rajmus Hojland mshambuliaji wa klabu ya Atalanta raia wa kimataifa wa Denmark ambaye amekua akifanya vizuri kwenye klabu hiyo lakini wamesimamisha dili hilo kwajili ya kukamilisha dila la Andre Onana.Man UnitedAndre Onana amekua kipaumbele zaidi kwa klabu hiyo baada ya kufanikiwa kumsajili Mason Mount, Lakini pia wanatafuta mshambuliaji mwenye ubora mkubwa lakini Onana amekua kipaumbele zaidi kwa klabu hiyo.

Man United wanatarajiwa kumalizana na Onana ndani ya wiki na kutangazwa kama golikipa mpya wa klabu hiyo baada ya David de Gea kutimka klabuni hapo na baada ya hapo ndipo watahamishia nguvu kwa mshambuliaji.Man UnitedRajmus Hojland ambaye yupo kwenye orodha ya juu kabisa katika washambuliaji wanaohitajika na klabu ya Man United, Huku amaslahi binafsi baina ya mchezaji na klabu hiyo yakielezwa sio tatizo kinachosubiriwa ni Mashetani wekundu kutuma ofa kwa klabu ya Atalanta.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.