Klabu ya Manchester United imethibitisha na kutangaza kuondoka kwa kiungo wake wa pembeni Jesse Lingard kwenye klabu hiyo kwa uhamisho huru makataba wake utakapokoma mwezi ujao.

Jesse Lingard ameitumikia klabu ya Manchester United kwa miaka zaidi ya 20, mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza na zao la akademi ya mashetani wekundu na kwa misimu kadhaa alikuwa ni moja ya mchezaji wa pembeni bora kwenye klabu hiyo.

Lingard msimu wa 2020-21 alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya West Ham United, baada ya nafasi yake kuwa finyu kwenye kikosi cha mashetani wekundu, na akiwa kwenye klabu hiyo ya London aliweza kuonesha kiwango bora msimu huo.

Msimu wa 2021-22 alirejeshwa kwenye klabu ya Manchester United, alishindwa kucheza kwenye kiwango cha juu licha ya kucheza kwenye kiwango cha juu msimu wa 2020-21 akiwa West Ham, na amefanikwa kuanza kwenye michezo miwili tu ya Ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Man United imeshafanya mazungumzo mara mbili na Lingard ya kutaka kumpa mkataba mpya, lakini pande hizo mbili hazikuweza kufikiana makubaliano ya kimaslai.

Taarifa ya Lingard imetoka baada ya klabu ya Man United kutangaza kuacha na kiungo wake Paul Pogba ambae nae anaondokwa kwa uhamisho huru.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa