Manchester United Yamvizia Beki wa Sporting CP

Klabu ya Manchester United imeingia vitani kumuwania beki wa kati wa klabu ya Sporting CP ya nchini Ureno anayefahamika kama Goncalo Inacio, Beki huyo anefanya vizuri kwasasa klabuni hapo.

Manchester United wana mpango wa kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ulinzi katika dirisha dogo la usajili, Huku jina la beki Goncalo Inacio likiingia kwenye orodha ya mabeki wanaohitajika klabuni hapo.manchester UnitedGoncalo Inacio mwenye umri wa miaka 22 mpaka sasa amekua kwenye ubora mkubwa ndani ya klabu ya Sporting CP kiasi cha Man United kuvutiwa na ubora wake na kuanza kumnyatia ili kupata saini yake.

Mashetani wekundu wanaelezwa walikua na mpango wa kusajili beki wa katikati katika dirisha kubwa lililopita, Lakini mpango huo ulivurugika kutokana na kiwango cha pesa kilichokua kinahitajika na vilabu ambavyo waliwahitaji wachezaji wao.manchester UnitedManchester United wanaandamwa na majeraha katika safu yao ya ulinzi kwasasa ambapo inaelezwa ndio sababu kubwa ya wao kutaka kuhakikisha wanaingia sokoni mwezi Januari kusajili beki kwajili ya kukipa nguvu kikosi chao, Wachezaji wanaotajwa sana ni Goncalo Inacio, Jean Clair Todibo, pamoja na Edmond Tapsoba.

Acha ujumbe