Klabu ya Manchester United imefanikiwa kupindua meza kibabe baada ya kuifunga klabu ya Brentford baada ya kutoka nyuma na kufunga mabao mawili na kushinda mchezo huo.
Manchester United walitoka nyuma ambapo walitanguliwa kwa bao la mapema lilifungwa na kiungo wa Brentford Jensen baada ya kiungo Casemiro kupoteza mpira na kusababisha bao hilo.Man United ilienda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao moja kwa bila lililofungwa mapema kipindi cha kwanza,Klabu hiyo ilirejea kipindi cha pili kwa kasi wakifanya mashambulizi zaidi kwenye lango la Brentford lakini milango ya Brentford iliendelea kua migumu.
Kocha Erik Ten Hag alifanya mabadiliko ambayo yalimlipa kwa kiasi kikubwa pale ambapo alimtoa kiungo Sofyan Amrabat dakika ya 87 na kuingia Scott Mctominay ambaye alikua shujaa wa mchezo huo, Mctominay alifanikiwa kufunga mabao mawili katika dakika za nyongeza goli la kusawazisha akifunga dakika ya 93 na bao la ushindi akifunga dakika ya 97.Manchester United sasa inafanikiwa kushinda mchezo wake wa nne wa ligi kuu ya Uingereza kati ya michezo nane ambayo wamecheza mpaka sasa, Klabu hiyo imefanikiwa kufikisha alama 12 klabu hiyo imekua na mwanzo mbaya sana msimu huu.