Kiungo wa zamani wa vilabu vya Chelsea, Lille, na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya taifa ya Ubelgiji Eden Hazard ametangaza kustaafu soka rasmi akiwa na umri wa miaka 32 tu.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram Hazard ameeleza kua ameona huu ni wakati sahihi wa yeye kuachana na mchezo huu na kuangalia mambo mengine nje ya mpira wa miguu.Kupitia Instagram Hazard amesema “Kuna Muda unajisikiliza na unasema acha wakati sahihi. Baada ya miaka 16 na kucheza zaidi ya Michezo 700 nimeamua kustaafu. Niliweza kutambua kipaji changu, nikacheza na nikawa na wakati mzuri kwenye viwanja vingi duniani, wakati wa career yangu nilipata bahati ya kukutana na wachezaji na Makocha wakubwa Asanteni wote kwa kua na wakati mzuri na ninawakumbuka sana Pia naomba nishukuru vilabu ambavyo niliwahi kuvitumikia LOSC, CHELSEA, Real Madrid na Belgium. Asante kwa Familia yangu, marafiki, washauri na watu waliokua karibu na mimi kwenye nyakati nzuri na mbaya. Mwisho, Asante sana mashabiki ambao mmekua na mimi kwa miaka yote hiyo mlikua mkinihimiza na kunisukuma kujituma zaidi Sasa ni muda wa kupumzika na kupata uzoefu mpya Tutaonana hivi karibuni rafiki zangu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amefanikiwa kuweka rekodi tofauti tofauti akiwa mchezaji na kushinda mataji kadhaa kama mchezaji, Kwani kiungo huyo amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza, mchezaji bora wa ligi kuu ya Ufaransa, mchezaji bora wa msimu wa michuano ya Europa, mchezaji bora wa mwaka Ubelgiji mara tatu 2017,2018,2019 na tuzo nyingine nyingi.Kiungo Eden Hazard pia amefanikiwa kutwaa mataji lukuki akiwa mchezaji ambapo amefanikiwa kushinda ligi kuu ya Ufaransa akiwa na Lille 2010/2011 ligi kuu ya Uingereza mara mbili msimu wa 2014/15 na 2016/17 kombe la Europa league mara mbili 2012/13 na 2018/19 akiwa na Chelsea, ligi ya mabingwa ulaya akiwa na Real Madrid msimu wa 2021/22 kombe la La Liga 2019/20 na Uefa Super Cup 2022.