Marcus Rashford Arejea Mazoezini United.

Mshambuliaji nyota wa Manchester United, Marcus Rashford, ameonekana mazoezini wakati timu hiyo ikijiandaa na muendelezo wa EPL wikiendi hii.

Rashford alifanyia upasuaji wa bega mwezi Julai na taarifa rasmi kutoka United, ziliripoti mchezaji huyo atarejea uwanjani mwishoni mwa mwezi Oktoba au mwanzoni mwa mwezi Novemba, 2021.

Kurejea kwa Marcus Rashford wakati huu, ni mapema kuliko ilivyokuwa imetarajiwa. Hii ni ishara nzuri kwa Ole Gunnar Solskjaer na kikosi cha United kwa ujumla. Japokuwa, bado ni mapema kumuona Rashford uwanjani, mashabiki wa The Red Devils wategemee kumuona mchezaji huyu muda mfupi ujao akichuana na washambuliaji wenzake kwenye kikosi cha timu hiyo.

Lindelof, Pogba na Rashford wakiwa mazoezini.

Manchester United watasafiri wikiendi hii kuwafata West Ham United pale London Stadium katika muendelezo wa EPL. Timu hizi zitakutana tena Jumatano wiki ijayo kwenye mzunguko wa 3 wa Carabao Cup kabla ya United kuwaalika Villareal kwenye mchezo wa 2 wa Ligi ya Mabingwa – Uefa.


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe