Neymar inasemekana ameuambia uongozi wa Madrid kwamba endapo wanamhitajinkikosini hapo kwa sasa hawana budi kufanya baadhi ya mambo ambayo yeye anaonelea yatakuwa na tija kwake na kuleta mafanikio ndani ya kikosi hicho. Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na kutaka kuihama klabu yake ya PSG na kutaka kurudi zake Hispania kuendeleza ushindani katika ligi hiyo. Baadhi ya mambo yaliyowekwa mezani ni kama vile:
Ameitaka klabu hiyo kuwabakiza kikosini hapo wachezaji kama Casemiro, Vinicius Jr., Rodyrgo kutoka Santos (aliyojiunga nayo Juni), pia anapenda kufanya kazi na Isco. Hawa amewataka waendelee kusalia kikosini hapo maana anajua uwezo wao upoje. Mbali na hao pia amewataka waweze kumshusha Roberto Firmino kutoka Liverpool na Miltao kutoka Porto.
Baadhi ya wachezaji walitajwa waliwahi kuhusishwa kutaka kusajiliwa na kiamba hao kipindi cha hivi karibuni japo, kuna wengine litakuwa ni suala la mtihani mzito kwa Perez kuweza kuwashusha kikosini hapo; kwa sababu ni suala la bajeti kubwa sana isiyo ya kawaida ikijumuishwa na kiwango kitakachohitajika kumsajili Neymar mwenyewe.
Kama Neymar atakubali kusaini Los Blancos ni uhakika kwamba atakuwa amewasaliti kwa kiasi kikubwa Barcelona ambao ndio wamemlea kwa kiasi kikubwa. Maana kwa mazingira aliyoondoka klabuni hapo yalikuwa ni yenye utata na kashkashi nyingi na hadi anaondoka klabuni hapo uongozi wa juu wa mabingwa hao haukuamini kabisa kama angeweza kuondoka kwa wakati ule.
Japo Madrid kwa sasa wapo katika hatua za kujaribu kurudisha heshima kikosini hapo kwa kutafuta nyota atakayeweza kuibeba timu wakati ikiwa inahitaji matokeo muhimu wakati wowote tangu walipomkosa nyota wao wa muda wote, Ronaldo ambaye alitimka kikosini hapo baada ya kuwapa vikombe na matokeo yote muhimu klabu hiyo.
Kwa sasa wamekuwa wakitapatapa kutafuta mbadala huo na hatuoni kama Madrid wanaweza kukataa ofa ya kumsajili mchezaji huyo. Kwa sasa kilichobaki ni kukamilisha masharti ya anayoyataka mchezaji huyo au yeyote yule ili kuweza kutimiza matakwa ya kukijenga kikosi chao ambacho kimekosa mwenendo unaoeleweka kwa kipindi kirefu.
Ni wakati ambao wanahitaji utulivu wa hali ya juu ili kuweza kupata mchezaji anayeweza kuwa mbadala sahihi. Japo machaguo yote yanaweza kuwa sahihi endapo watafanikiwa kuwanasa maana wametega rada zao kutaka kumnasa aidha Neymar au Hazard ambao wote wana uwezo mkubwa japo; kwa mahitaji ya timu Hazard pekee anaweza kuendana na mfumo, hii inatokana na kasi aliyonayo na maamzi ya haraka kuweza kuutumia mpira akiumiliki. Hili pekee linaweza kuwa mwarobaini wa tatizo lililopo kwa sasa kikosini hapo. Tunahitaji kuiona Madrid ile ya makombe kwa sasa kwq sababu wamekuwa wakionekana kusuasua kwa kiwango kikubwa kitu ambacho ni hatari kidogo.


isha
Neymar uko vizuri