Pambano Dhidi ya Nurmagomedov Lazima!

Conor McGregor amerejea kwa mbwembe za aina yake akitamba kuwa mechi ya marudiano dhidi ya mpinzani wake Khabib Nurmagomedov haikwepeki!

McGregor ameweza kumkalisha mpinzani wake Donald Cerron ‘Cowboy’ kwa KO ndani ya sekunde 40 tu pale Las Vegas. Hili lilikuwa ni pambano la kwanza la McGregor tangia alipochapana na Khabib Nurmagomedov Oktoba 2018.

Akizungumzia pambano la marudio dhidi ya Khabib, McGregor anasema pambano lazima liwepo akisinasibu kuwa kwa sasa yuko kwenye fomu nzuri ukilinganisha na mara ya kwanza.

Baada ya McGregor kurejea kwa ushindi, Floyd Mayweather aliibukia kwenye kurasa zake na kuchapisha kuwa anatazamia kurejea kutoka kustaafu kwake kwa mechi ya marudiano dhidi ya bondia huyu. Alichapisha picha iliyotaja pambano lake dhidi ya McGregor 2020.

 

Hata hivyo, kwa upande wa Nurmagomedov, tangia alipopambana na McGregor hajapoteza pambano hata moja na anatarajia kupambana na Tony Furgerson kutoka USA mwezi April 2020 kwenye UFC 249.

Pambano la marudio kati ya McGregor na Nurmagomedov, linatarajiwa kuwa pambano kubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa ndondi.

2 Komentara

    Sawa mkali uko vizuri

    Jibu

    Mc Gregor ni mpiganaji mzur sana lakn tatizo lake n moja anadharau sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.