La Liga iliendelea wikiendi na mechi kadhaa zilikuwa kama hivi hapa chini:
Real Madrid v Eibar
Real Madrid wameshinda 3-1 dhidi ya Eiber katika mechi iliyochezwa kwenye dimba la Alfredo di Stefano. Hii ni mechi ya kwanza kwa ya kimashindano kwa Real Madrid baada ya ligi kuwa ilisimamishwa kwa miezi takribani mitatu kwa sababu ya janga la Covid-19.
Goli la kwanza la Madrid lilifungwa na Toni Kroos mnamo dakika ya nne tu ya mchezo kabla nahodha Sergio Ramos hajafanya hivyo dakika 26 baadae. Goli la tatu liliwekwa kimiani na Marcelo katika dakika ya 37 ya mchezo.
Eiber walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji wao nyota Pedro Bigas baada ya kumalizia shuti la mshambuliaji Segi Enrich liligonga mwamba.
Ushindi huo kwa Real Madrid unaifanya timu hiyo kusalia nafasi ya pili ya msimamo wa La Liga na alama zao 59 baada ya kuwa wamecheza michezo 28 mpaka sasa, alama mbili nyuma ya Barcelona wanaaongoza msimamo wa ligi hiyo.
Atletico Madrid v Athletic Bilbao
Mchezo huu uliisha kwa sare ya kufungana 1-1. Kwa matokeo hayo Atletico Madrid wanasalia katika nafasi ya sita ya msimamo.
Goli la Atletico Madrid lilifungwa na Diego Costa, na kuwa goli la kwanza kwa nyota huyo kwa mwaka huu. Diego Costa alilitoa goli hilo kama zawadi kwa mchezaji wa timu ya wanawake ya Atletico Madrid, Virginia Torrecilla, baada ya midfielder huyo kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe katika ubongo mnamo mwezi May.
Athletic Bilbao walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa nahodha wao Iker Muniain katika dakika ya 37 ya mchezo kabla Diego Costa hajasawazisha dakika mbili tu baadae.
Real Sociedad v Osasuna
Sare ya 1-1 ndiyo matokeo ya mchezo huu.
Kwa matokeo hayo, Real Sociedad wanasalia nafasi ya nne ya msimamo wa La Liga wakiwa na alama 47, alama moja zaidi ya Getafe wanaoshikilia nafasi ya tano. Huku Osasuna wakiwa nafasi ya 11 ya msimamo na alama zao 35.
Goli la Real Sociedad lilifungwa na Mikel Oyarzabal huku lile la Osasuna likiwekwa kimiani na Adrian Lopez kwa mkwaju wa penati.


Magdalena
Real madrid ilikuwa poa Sana ilijua kunipatia mzigo wa maana
Neema juma
Real Madrid ndomaana naipendagaa wako vizuri
Mwanaidi
Madrid wako vizuri sana aisee ndio mana wamefanya vizuri
Tahiya
Real Madrid hakika sijakosea kwenye kubetia hii timu mana imefanya siku yngu kuwa njema kabisa
Ester mmakasa
Real Madrid hongera sana kwenu kazeni buti ili muwe vizuri mwishoni mwa ligi.
felister
ahsante atletico madrid kwa kunipa ela ckukosea nilivyoweka Gg
Johnmary joel
Matokeo haya yananipa raha Madrid hongeren sana songeni mbele zaid#meridianbettz
Furahav
Haya ndo tulikuwa tumemisi.
Leonard
Hongera Real mardid
Kenani
Madrid wamepiga mpira kisawa sawa
Zeiyana
Tumeona kazi yao Madrid kwa kipindi kifupi cha mapunziko ya kolana kweli kuna watu mpira hanaipenda toka moyoni safi sana Madrid sisi kama mashabiki tumefurahi
warda
Asanteni Meridian bwana nimepata Mpunga kiasi chake#Meridianbettz
Hamidu
Asante kwa update za michezo# meridianbettz.
David Pere
Bado matokeo yalikuwa so ya kulizisha sanaa yametubanaa
Frank Patrick
Bilbao na Atletico Madrid ilikuwa bonge moja la match
Genia Sikaluzwe
Real Madrid hongera kwa ushindi
Dorophina
Ndio tulikuwa tunasubilia mambo mazuri km hayo
Evaluziga
Real Madrid hongera kwa ushindi
lombo
Madrid jesh
Emmy cleopa
Ahsante kwa taarifa meridianbettz
Gabriel
Nice update 👍 #meridianbettz
Antony Luseno
Kwa anayeongoza ligi aendeleze ubabe wake
Caroline
Asanteni Kwa taarifa meridianbet
isha
Real madeid ndio maana naipendaga
Lydia Emmanuel Magoti
Safiii Sana Real Madeid wameupiga mpira kisawasawa
Julieth
Kulipooza sana sasa nu bull bull
Adelta
Hongera kwa real Madrid
Povel
Ilikuwah cku mbaya sana Sevilla kachana jamvi langu thnks meridian bet kwa update za michezo
Ester jackson
Mkeka wa hela nyingi Leverkusen ameuwa imeniuma sana
Hope mwaikuka
Duh sielew kabsa
Shafii
Gud newz
Elika
Habari njema hii
Samiah
Gud news kwa meridianbet
Hilda
Ndio mana naipenda madrid sio kwa.mshiko huuuu
Asia Abdy
Habar njemaa hzo
Khadija
Habari njema kwetu#meridianbettz
Neema hassan
Real madrid wako vizuri
Devotha
Asanteni sana kwa taarifa
Salma
Aya mambo tuliyamisi
Ernest
Nafurahi kuona ushindani ulivyokuwa mkubwa kwa upande wa kutwaa taji kati Barca na Madrid
Fatina mfingi
Asanteh meridianbet kwa taarifa
Tatu
Hongera Madrid