Bayer Leverkusen v Schlake 04
Bayer Leverkusen wamelazimishwa sare ya 1-1 na wachovu Schalke 04. Matokeo hayo yanawafanya Leverkusen wafikishe alama 57 huku wakiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Bundesliga huku wakibakiwa na michezo minne ya ligi hiyo.
Kwa upande wa Schlake 04 wao matokeo hayo yanawafanya waweke rekodi mbaya kwa timu yao kwa kutokushinda katika michezo 13 mfululizo ya Bundesliga kila mara wakiwa na sababu tofauti tofauti lakini kwa mechi hii lawama nyingi zitamuendea mlinzi wao Juan Miranda aliyejifunga dakika za jioni kabisa za mechi hiyo.
Schlake 04 walikuwa wanaelekea kushinda mechi hii kutokana na goli walilolipata mapema mwanzoni mwa kipindi cha pili. Hali ilibadilika katika dakika ya 81 baada ya Miranda kujifunga na kufanya mchezo huo uishe kwa sare ya 1-1.
Mainz v Augsburg
Pamoja na ushindi wa ugenini wa goli moja bila, Augsburg bado wapo katika hatari ya kushuka daraja. Hatari hiyo ni kubwa zaidi kwa Mainz waliokubali kipigo hicho cha goli 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani. Matokeo hayo yanawapeleka Augsburg nafasi ya 13 ya msimamo wakiwa na alama 35 huku yakiwaacha Mainz katika nafasi ya 15 na alama zao 31.
Goli pekee la Augsburg katika mchezo huo lilifungwa na Florian Niederechne katika dakika ya kwanza tu!
Mpaka sasa, Bayern Munich wanaongoza msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 73. Borussia Dortmund wanafuatia na alama zao 66. Kama Bayern wakishinda mechi yao ya Jumanne ya June 16 dhidi ya Werdee Bremen watafikisha jumla ya alama 76 hivyo ktawazwa mabingwa wa Bundesliga kwa mara ya tisa mfululizo!


Magdalena
Uku nako bundesliga kulinoga Sana ingawa kulikuwa kugumu kidogo
Neema juma
Hii ndohabariii tunazozitakaaa kwa kweli
Tahiya
Hapo ndio unajua nani kapanda kwenye msimamo wa ligi
Mwanaidi
Asanteni kwa taarifa za matokeo meridian
Ester mmakasa
Kila lakheri Bayern ,mungu awapiganie mfanye vizuri .
felister
safi Bayern munich
Johnmary joel
Bayern munich hongeren sana endeleeni vizuri#meridianbettz
Furahav
Kweli mpira hauna mwenyewe.
Leonard
Bayern munich bingwa
Kenani
Noma sana kwel mpira dakika 90s
Zeiyana
Daaah..!kweli mpira hauna mwenyew
Hamidu
Asante kwa taarifa#meridianbettz
warda
Mainz wameniangusha sana #Meridianbettz
David Pere
Matokeo sioazuri Sana kwa sisi wazee wa kutafuta pesaa
Frank Patrick
Liverkusen game ilikuwa ngumu sana kwao 04 walikaza sana
Genia Sikaluzwe
Bayern Munich noma
Dorophina
Dhaa wameniangusha mpaka mkeka wng umekufa
Theonestina
Kila la kheri bayern
Evaluziga
Du kweli mpira Haina mwenyewe
lombo
habar mzur
Emmy cleopa
Habar nzuri
Gabriel
Mtanange ulikuwa wa kibabe hatar
Antony Luseno
Kwa ligi hii adi sasa bingwa ashajulikana
Caroline
Asante meridian Kwa taarifa
isha
Bayern mkali nilijua tuu kwamba atashinda
Lydia Emmanuel Magoti
Duu kweri mpira dakika 90 izozingine wanajua waho
Adelta
Asante kwa taarifa # meridianbet
Povel
Dah jamvi langu limechanikah kikatil sana thnks meridian bet tz kwa update
Ester jackson
Leverkusen amenikera sana amechana mkeka wangu
Rehema
Habari mzuri
Hope mwaikuka
💪💪 bayern
Theckla
Munich wanatisha
Shafii
Asante kwa taarifa
Elika
Hongera kwa mechi zote zilizopata ushindi
Samiah
Munichi niwakali sanaaa
Asia Abdy
Asanten kwa kutujuza
Khadija
duuh mpila hauna mazoea#meridianbettz
Neema hassan
Bayern Munich jembee
Devotha
Asante kwa taarifa
Salma
Habari nzuri
Ernest
Bayern wanatisha sana msimu huu
farida ahmadi
Bayern Munich jeshii hanajua Sana mpira
Tatu
Good