Kiungo wa kimataifa kutokea Ufaransa aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Arsenal Matteo Guendouzi amejiunga na klabu inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Olympic Marseille kwa ada ya uhamisho ya £11milioni.

Matteo Guendouzi kuazia msimu wa 2020-21 alipelekwa kwa mkopo nchini Ujerumani kwenye klabu ya Hertha Berlin, ambapo alitumia mwaka mzima kwenye klabu hiyo, kabla ya kurejea Arsenal na kupelekwa tena Olympic Marseille kwa mkopo.

Matteo Guendouzi

Klabu ya Arsenal wakati wanamtoa kwa mkopo Matteo Guendouzi kwenda kwenye klabu ya Olympic Marseille majira ya kiangazi yaliopita msimu wa 2021-22, waliweka kipengere ambacho ikiwa klabu Marseille iatahitaji kumnunua basi itapewa kipaumbele.

Uhamisho wa Guendouzi umeigharimu klabu ya Marseille kiasi cha £11milioni, lakini kiasi hicho kinaweza kuongezeka ikiwa klabu hiyo itafanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Ufaransa.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa