Lionel Messi anaripotiwa kuwa atayari anamaliza uvumi uliobamba zaidi mwaka mzima juu ya maisha yake ya baadaye baada ya kukubaliana na kandarasi mpya ya miaka miwili na Barcelona.

Hatma ya mshindi wa Ballon d’Or mara sita imekuwa gumzo katika soko la usajili tangu alipojaribu kulazimisha kuondoka klabuni hapo msimu uliopita wa kiangazi, lakini baada ya mzozo kidogo kwa masuala ya kiutaratibu mwishowe alilazimika kusalia klabuni hapo.

Muargentina huyo hakufanya maamuzi juu ya hatma yake klabuni hapo wakati wa kampeni za 2020-21, hata hivyo, na Manchester City na Paris Saint-Germain walikuwa chonjo juu ya uamuzi wake wa kuondoka wakati mkataba wake ukiwa mbioni kumalizika mwisho wa mwezi huu.

Sergio Aguero na Lionel Messi
Aguero kukutana tena na Messi Barcelona.

Hata hivyo, ripoti huko Uhispania zimedai kuwa Messi amefanya mamuzi ya kusalia Hispania na kuendelea na Barcelona na hivi karibuni atasaini mkataba mpya na klabu hadi msimu wa joto wa 2023.

Kwa hivyo Messi amejiandaa kukamilisha maamuzi yake pamoja na Sergio Aguero huko Camp Nou kwa msimu wa 2021-22, na mshambuliaji huyo wa zamani wa Man City akijiunga kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka miwili.

Messi – ambaye atatimiza miaka 34 baadaye mwezi huu – alifurahiya kampeni nyingine nzuri huko Catalonia muhula uliopita, akifunga mabao 38 na kutoa usaidizi magoli 14 kwa mechi 47 za mashindano yote.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa