Messi Anukia Marekani

Gwiji wa zamani wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ambaye ameachana na klabu ya PSG ya nchini Ufaransa ananukia nchini Marekani kujiunga na klabu ya Inter Miami inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Lionel Messi imetaarifiwa amemalizana na klabu ya Inter Miami maslahi binafsi kwani aliondoka ndani ya PSG kwa uhamisho huru, Hivo kwasasa amefanya makubaliano ya kimaslahi baina yake na klabu ya Inter Miami na yuko tayari kujiunga na klabu hiyo.messiGwiji huyo alikua akifuatiliwa kwa karibu na klabu yake ya muda mrefu klabu ya Barcelona ili kuweza kumrudisha kwenye viunga vya Camp Nou, Lakini klabu ya Inter Miami iliyopo chini ya David Beckham wameweza kushinda mchuano wa kumchukua mchezaji huyo.

Lionel Messi amekua akifatiliwa pia na klabu ya Al-Hilal ya nchini Saudia Arabia ambapo taarifa zinasema amekataa ofa yao na kuamua kujiunga na klabu ya Inter Miami ya nchini Marekani, Huku vyanzo vikieleza inatokana na ushswishi wa familia yake na watoto zaidi wakihitaji kuishi Marekani zaidi ya Saudia.messiMashabiki wengi wa klabu ya Barcelona wameshtushwa na taarifa za Messi kujiunga na klabu ya Inter Miami, Kwani kwa asilimia kubwa waliamini mchezaji huyo atarejea ndani ya klabu ya Fc Barcelona na kuendelea kukipiga kwenye klabu yake ambayo ameitumikia kwa muda mrefu zaidi lakini imeshindikana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.